Kiongozi Mwanakijiji;
Inapokuja suala la Opportunity na Maslahi ya taifa, chaguo liko wazi.
In addition, dis is typikal in ma kinda a country. SICK!
1:
.kuhusu wizi wa mabilioni kwa kutumia makampuni ya Meremeta,
Mwananchi Gold, Deep Green Finance na Tangold hatuna budi kujua kuwa wizi huu ulipangwa na kuendeshwa kwa umakini mkubwa lakini
pia umekuwa ni mtego mkubwa kwa serikali kwani baadhi ya watu
waliohusika au kunufaika kwa kiasi kikubwa wamo ndani ya serikali hiyo hiyo. Waziri Masha ni mshirika katika kampuni ya mawakili ya
IMMMA ambayo mawakili wake wengine wawili ndio walionekana
kama wakurugenzi katika kampuni ya Deep Green Finance.
2:
Lakini pia cha kushangaza na kushtua zaidi ni pale ambapo washirika wawili (patners) wa kampuni ya IMMMA mmoja anateuliwa
kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani (baadayeWaziri kamili) na mwingine anateuliwa kuwa Jaji licha ya wingu hili la wizi wa Benki
Kuu likiwa bado limeizunguka kampuni hiyo.
3:
Vile vile kilichoshtua zaidi ni taarifa iliyochapishwa na gazeti la MwanaHalisi kumtaja kuwa mtoto wa Rais Kikwete ni mshirika kwenye kampuni hiyo ya IMMMA. Habari hizo zilipotangaa hakuwa mwingine isipokuwa Waziri Masha aliyejitokeza na kumtetea Ridhiwan Kikwete
licha ya ukweli kwamba yeye (Masha) yuko likizo toka shughuli za
kampuni ya IMMMA! Maswali yaliulizwa wakati ule ni kwanini Masha azungumzie mambo ya kampuni binafsi badala ya kuacha watu wa IMMA
kujibu tuhuma dhidi yao isipokuwa ni kwa sababu ya madaraka aliyokuwa
nayo?
4:
je ni sababu zipi ziliwafanya wageni hao kuzitoa Benki kwa cash na walizipeleka wapi?)Uzito wa fedha zilizohamishwa tarehe 1Agust kwa fedha taslimu ni sawa natani 50 yaani uzito sawa na lori 5 za tani kumi
kumi). Je ni utaratibu fedha za umma kuchukuliwa kwa mtindo huo?
5:
Ni wazi kwamba kati ya mambo ya kutisha na makubwa zaidi na yenye utata ni suala la Meremeta, Mwananchi Gold, Deep Green Finance na Tangold. Ni wazi uchunguzi mkubwa zaidi na huru unahitajika kufanyika. Hata hivyo kutakuwa na ugumu mkubwa wa kuupata ukweli kwani baadhi ya watu ambao wanatakiwa kuhojiwa ndio walioshikilia nafasi ambazo zinahusika na uchunguzi huu. Kama suala moja la EPA limechukua miaka miwili kuweza kuanzisha kamatakamata na hatimaye watu kuanza kufikishwa mahakamani je masuala ya Meremeta, Deep Green Finance,Mwananchi Gold na Tangold yatachukuamuda gani? Na hapa hatujaleta masuala ya Bank M!