Wakili Masha alinufaikaje na Deep Green Finance?

Nimekumbuka ulichoandika mkuu, inasikitisha lakini kuna hatma ya haya yote!
 
Kuna Madai kuwa Mzee wa Kaya ametoa hata Majaji toka katika IMMA na kwenda mahakama kuu, sasa unategemea nini

Mkuu Josh,

Si madai ni ukweli one of the senior partners wa IMMA aliteuliwa kuwa jaji wa mahakama kuu, hii sio siri hata kidogo!!!

Tiba
 
Duh kweli ni hatari tupu katika Tanzania, Kama kweli hawa wanafanya na kuibia Tanzania Mungu atawahukumu siku moja
 
mtoto wa nyoka ni nyoka....mlitegemea Ridhiwani afanye nini tofauti na mkulu??
 
Kuna mengi sana katika haya mambo tutaona mengi sana kuliko unavyoweza kudhani Mzee wangu Mm Mwanakijiji
 
Hivi kweli katika Nchi inayoata sheria Waziri mkubwa ametajwa katika tuhuma za wizi wa kampuni ya Deep green Finance,bado tu yupo madarakani,ile kutajwa tu na ni kweli kuwa alikuwa kwenye kampuni hiyo alitakiwa aachie ngazi au Rais amwajibishe.Jamani Tanzania tutafuata lini sheria katika Uongozi?
 
IMMA Advocates hiyo hiyo pia iliiwakilisha Tangold, kampuni iliyoirithi Meremeta. Hivi sasa serikali imepiga marufuku kujadiliwa kwa Meremeta kwa sababu eti ya Usalama wa taifa !!
 
Ingekuwa na Watu makini na Vyama makini na Utawala makini Masha muda mrefu angekuwa hana Uwaziri na amefungwa siku nyingi
 
Kiongozi mzuri ni yule anayeachia ngazi akiwa na tuhuma kupisha uchunguzi.
 
Vijana hamjishughulishi mnajambajamba hapa na hisa 1% za Masha,Endeleeni,ya anakula vya ndani
 
IMMA Advocates hiyo hiyo pia iliiwakilisha Tangold, kampuni iliyoirithi Meremeta. Hivi sasa serikali imepiga marufuku kujadiliwa kwa Meremeta kwa sababu eti ya Usalama wa taifa !!
MKUU SALAMA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…