Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju amewataka wanawake kujitokeza kwa wingi kwenda kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi mkuu utakafoanyika mwaka huu.
Akizungumza katika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Kanda ya Kusini linalofanyika wilaya ya Nachingwea, Mkoa wa Lindi, Mpanju amesema kuna umuhimu wa nafasi kujiamini na kuchukua hatua za kuwania nafasi za uongozi.
"Wanawake ni chachu ya maendeleo wamekuwa mhimhili na chachu ya maendeleo ya taifa naomba mjitokeze mara kipyenga kitakapolia jitokezeni nendeni mkachukue fomu gombeeni nafasi za udiwani gombeeni nafasi za ubunge" amesema Mpanju
Aidha amewataka kujiamini kwani tayari kuna mifano ya viongozi walioshika nyadhifa na kuonyesha mafanikio makubwa.
"Na mfano mzuri ni Mheshimwa Rasi Dkt. Samia Suluhu Hassan, Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson na Msajili mkuu wa Mahakama Eva Nkya chukueni fomu mshiriki kwenye kuamua na kupanga mstakabali wa taifa letu"