Siku ya jana akiwa anazungumza kwenye mdahalo ulioandaliwa na Jamii Forums pamoja na Star TV, Wakili Boniface Mwabukusi amedokeza kuwa yuko mbioni kufungua kesi dhidi ya vyama 14 vya upinzani nchini
Akiwa anazungumza mbele ya Chief Odemba wa Star TV, Mwabukusi alisema kuwa atafungua kesi ambayo italazimisha vyama hivi 14 vifutwe kwani vimekuwa vikileta vurugu na ukandamizaji wa mchakato kidemokrasia nchini.
"Hivi vyama 14 binafsi nafikiria kutaka kufungua kesi vifutwe kwa sababu nataka kuomba nadhani mpaka wiki ijayo ntakuwa nimekamilisha, nataka kuomba nione ripoti zake za perfomaance ya vyama hivi kama kweli vinahitajika kuwepo kwa sababu vyama hivi vinaleta vurugu katika nchi"
vifutwe vyote hata ccm, tupate au tutafute utaratibu mpya wa kujiongoza na mambo yetu. vyama vyote vimeshindwa kazi mpaka sasa ni malumbano tu kwenda mbele, mfano dira ya taifa isiyosema mkakati wa lini tutakuwa self sufficient hata katika kitu kimoja kama chakula, afya etc, malumbano ya tunakopesheka, malumbano ya PPP na kafulila wake, yaaani malumbano kila kona. Hatujui tunataka nini, lini na namna gani ya kukitaka hicho tunachokitaka kama nchi. wengine sasa wamefikia lengo lao la liwalo na liwe tu bila hivi figusu za vyama na malumbano yao madaraka.
Labda tukiamua kwamba viongozi wa umma wote- walipwe mishahara kama ya walimu, ndio watu/viongozi watajitambua. Huduma kwa jamii si anasa, ni kujituma tu na sio kujimwambafai na ma V8. Kukimbilia anasa ndio chanzo kikuu ca matatizo yetu, kila sehemu, watu wanataka utajiri wa haraka bila kazi- kamari kila kona, tatu mzuka na mengine mengi...
watawala wetu/ viongozi wetu kwa kweli jitafakalini kwa namna mlivyo tufikisha hapa. Hata Mungu ana tabi ya kubadilisha viongozi akiona watu wake wanayumba, hatuwezi kuwa static ingawaje muumbaji wetu ni dynamic na mifano ni Mingi.