Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakili Mwanaisha Mndeme ambaye ni Katibu wa Idara ya Mambo ya Nje ya ACT Wazalendo, na Waziri Kivuli Viwanda na Biashara wa chama hicho, leo tarehe 6 Februari 2025 ametangaza nia ya kugombea ubunge wa Jimbo la Kigamboni mkoani Dar es Salaam katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Wakili Mndeme amesema atahakikisha changamoto zote za Wanakigamboni zinatatuliwa hasa suala la barabara na usafiri lakini pia kama mwanasheria, atahakikisha suala la ardhi kwa Wanakigamboni analishikia bango kwa kuwa ndilo tatizo kubwa kwao.
Soma pia: Waziri Kivuli wa ACT Wazalendo Ndolezi Petro atangaza nia ya kugombea Ubunge jimbo la Kigoma Kusini
Source: Jambo TV