Wakili mzawa anapomtetea raia wa kigeni anayehujumu taifa letu

mmteule

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2011
Posts
5,883
Reaction score
14,600
MaWakili wanatetea wavuvi haramu toka nje ya nchi, Wakili wanatetea wauaji wa albino, wakili wanatetea raia wa nje waua tembo wetu, wakili wanatetea wala rushwa wakubwa za EPA, NDEGE YA RAIS, BOT na leo nimesoma hii nikahamaki....

"Raia Watatu wa China, Huang Gin, Xu Fujie na Chen Jinzha wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam,washtakiwa hao wanadaiwa kukutwa wakiwa na nyara za serikali aina ya pembe za ndovu, shehena ya Pinde 706, vyenye uzito wa kilo 1880 zikiwa na thamani ya Sh5 bilioni. Washtakiwa hao, kupitia kwa mawakili wao, Edward Chuwa na Richard Rweyongeza waliwasilisha maombi ya dhamana Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, wakiomba wapewe dhamana, baada ya Mahakama ya Kisutu kuwanyima dhamana kutokana na kutokuwa na uwezo wa kisheria kusikiliza kesi hiyo". source mwananchi ya leo 5/2/2014.
Jamani mawakili wazawa....mnisaidie mimi na watanzania tusiojua
1. Ni kesi zipi msizoruhusiwa kutetea watuhumiwa?
2.Je kama wewe ni wakili na nimekuibia mali yako binafsi unaweza pia kusimama kunitetea? kama jibu ni hapana mbona
Kwa Taifa lako siyo hapana?
3. Je mawakili wanaamini katika Utaifa wa nchi ipi au nyinyi hamna Utaifa nyoyoni mwenu?
4. What are the donts ya mawakili?
5. Profesional ethics zenu ni zipi?
Nitashukuru kwa majibu yatakayokidhi haja, lakini pia yaambatane na ushahidi wa kanuni ama sheria rasmi. kazi kwenu kujitetea mbele ya Watanzania vinginevyo tutaendelea kuwalaumu bila.
Sio watuhumiwa wote wana makosa (hili jibu siitaji kuliona kwenye majibu yenu) ahsanteni!
 
Mawakili wana mambo, na hakuna kesi hata siku moja itakayokosa wakili. Wewe baka hapo hadharani, ushahidi wa picha uwepo, ukipelekwa mahakamani, bado watajitokeza mawakili kukutetea. Wanakataa hata ukweli
 
Kwani hao mawakili wao huwa wanatetea watu bure pasipo malipo ya pesa?
 
Pesa ni kitu mbaya sana. Yuda alimsaliti Yesu, nabii wa Mungu na kiongozi wake wa kiroho na maisha, kisa pesa. Wapo walioua wazazi au wanafamilia coz pesa. Na hao mawakili wapo tayari kuisaliti nchi yao coz pesa. Imani yao ni kuwa nchi yenyewe ishauzwa na wao wanamalizia vilivyobaki.
 
Ni haki ya msingi kuwa na mwanasheria wa kukutetea mahakamani. Hui haijalishi mzawa au RAIA wa kigeni.
 
Ni haki ya msingi kuwa na mwanasheria wa kukutetea mahakamani. Hui haijalishi mzawa au RAIA wa kigeni.

mbona hujibu hoja zilizoulizwa, au wewe sio wakili msomi Mkuu?
 
Sheria ni taaluma kama zilivyo nyingine,pamoja na mambo mengine wanasheria wanaingia mikataba na clients zao kabla hajaingia mahakamani kudefend, hivyo basi sioni tatizo wakili kutetea whether mzawa ama asiyekuwa mzawa as long anasimama kwenye haki!
 
NI haki ya binadamu yeyote yule kutetewa, haijalishi ni RAIA wa nchi gani . Lila mtuhumiwa lazma atetewe kwa sababu zifuatazo

1.NI muhimu kutetewa ili hata kama kweli ana kosa basi WAKILI anasaidia yule mtu apewe adhabu inayolingana na kosa lake

2.NI haki ya kila mtu kusikilizwa na kujitetea kwa kosa analotuhumiwa nalo, na kuwa mawakili ni wataalamu wa sheria ni haki kwa mtu huyo kusaidiwa kujieleza kitaalam ili haki itendeke kwake.

3.mawakili ni ma afisa wa mahakama hivyo basi wako pale pia kuisaidia mahakama kutenda haki.
 
Sheria ni taaluma kama zilivyo nyingine,pamoja na mambo mengine wanasheria wanaingia mikataba na clients zao kabla hajaingia mahakamani kudefend, hivyo basi sioni tatizo wakili kutetea whether mzawa ama asiyekuwa mzawa as long anasimama kwenye haki!

Dahh...inaniuma sana kuona mjomba akiwatetea wale Wachina waliokamatwa na meno ya tembo huko Mikocheni.
Any way..hiyo ni kada. Ninachoona, serikali ni dhaifu sana katika kusimamia kesi i.e kupeleleza na kutetea ushahidi, hivyo Mawakili wanaojituma hufanikiwa kiulaini hata kuwasidia wahalifu. Sitashangaa kusikia Wachina wa meno ya tembo - Mikocheni wametoka tunduni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…