Wakili Peter Madeleka, tayari amefika kwenye viunga vya Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Ardhi ambapo kesi inayowahusu waliokuwa wafanyabiashara 'wapangaji' kwenye jengo la ghorofa lililoporomo Kariakoo, Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwaka 2024 inaanza kusikilizwa leo, Jumatatu Mei 25.2026, ambapo 'wafanyabiashara' hao wanadai fidia ya takribani Bilioni 40 za Kitanzania kutoka kwa waliokuwa wamiliki wa jengo hilo
Wakili Madeleka ambaye anawawakilisha wafanyabiashara hao, amenukuliwa mara kadhaa akieleza kuwa fidia inayodaiwa ni kutokana na hasara za upotevu wa mali, raslimali fedha walizopata wataja wake, huku baadhi yao wakiwa wamepoteza maisha kutokana na ajali hiyo, ambapo wateja wake wanaamini kuwa kutokea kwa ajali hiyo kumechangiwa na uzembe wa waliokuwa wamiliki wa jengo hilo kwa namna moja au nyingine.