Wakili wa kesi ya UAMSHO aomba kesi kufutwa

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,575
[h=1][/h]


Salma Said,
MAHAKAMA ya Wilaya ya Mwanakwerekwe imeombwa kuifuta kesi inayowakabili viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) kutokana na kuchukua muda mrefu kwa kesi hiyo bila ya ushahidi wake kukamilika.
Wakili wa washitakiwa hao, Salum Toufik alimuomba hakimu anaeiendesha kesi hiyo, Ame Msaraka Pinja kwamba kutokana na taratibu za kimahakama hususan katika makosa ya jinai kesi inapokuwa imefikia kuanzia miezi mitatu na kuendelea bila ya upelelezi kukamilika inapaswa kufutwa.
“Mheshimiwa mimi nahisi ni muda mrefu sasa wateja wangu wapo rumande na kesi kila siku upelelezi haujakamilika naiomba mahakama yako tukufu iangalie sheria na kanuni ili iweze kuifuta kesi hii,” alisema Towfik.
Kesi hiyo inayowakabili viongozi hao wakiongozwa na Sheikh Farid Hadi Ahmed ambao wanadaiwa kutenda kosa la uchochezi wa kufanya fujo kinyume na kifungu cha 45 (1)(a) na (b) sheria namba 6 ya mwaka 2004 walifikishwa tena jana katika mahakama hiyo kwa kutajwa.
Upande mashataka awali umeomba muda zaidi kuendelea na upelelezi wa kesi hiyo.
Upnde huo ukiongozwa na Khamis Jafar wameiomba mahakama kuwapa muda zaidi baada ya upande wa watetezi wa washtakiwa kuiomba mahakama hiyo kuifuta kesi hiyo kutokana na kuwa imekuwa kipindi kirefu pasipo na upelelezi kukamilika.
Hata hivyo, hakimu wa mahakama hiyo aliiahirisha kesi hiyo hadi Machi 19 mwaka huu, kwa kutajwa na washitakiwa wamerejeshwa rumande hadi tarehe hiyo.
Washitakiwa hao ni Sheikh Farid Hadi, Mselem Ali, Mussa Juma, Azza Khalid Hamdan, Suleiman Juma, Khamis Ali na Hassan Bakari .
Mapema mwendesha mashtaka huyo alidai mahakamani hapo kuwa washitakiwa hao wakiwa ni wahadhiri kutoka Jumuiya ya Uwamsho na Mihadhara ya
Kiislamu walitoa matamko ya uchochezi yanayoashiria uvunjifu wa amani na kusasabisha fujo, maafa mbali mbali na mtafaruku kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na uharibifu wa mali za watu na serikali.
Wakati huo huo kesi nyingine inayowakabili viongozi wa Jumuiya ya Uamsho Zanzibar juzi ilitajwa mbele ya hakimu mpya baada ya Hakimu Mohammed Ali Shein kujitoa katika kesi hiyo ya kufanya fujo.
Hakimu Shein alijitoa Desemba 27 mwaka jana katika kesi hiyo inayowakabili Sheikh Farid Hadi na wenzake sita iliyopo Mahakama ya Mwanakwerekwe mjini Zanzibar.
Kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu wa Wilaya, Khamis Rashid ambapo washitakiwa wanne wako nje kwa dhamana na watatu bado wako mahabusu kutokana na kesi nyingine inayowakabli.
Washitakiwa watatu ambao walikwenda katika kesi hiyo wakitokea mahabusu ni Masheikh Farid, Juma Suleiman na Mussa Juma ambao wanakabiliwa na kesi Mahakama Kuu ya Vuga ambayo dhamana imefungwa.
Kesi hiyo ya Mwanakwerekwe inatarajiwa kutajwa Machi 4 na 5 na ile ya Mahakama Kuu itaendelea hapo kesho katika Mahakama ya Vuga Zanzibar.
 
Kwanini wasiombe na uamusho ufutwe? Watanzania tulizoea amani, lakini uamusho wameleta uhasama na chuki miongoni mwa wazanzibar na watanzania kiujumla!
 
Ni heri wahukumiwe kifungo cha maisha tu.
 
Inabidi watafute namna nyingine ya kuwa-pin hawa UHAMSHO, lakini si kwa style hii ya KITOTO. Hizi ni miongoni mwa kesi zisizokuwa na kichwa wala miguu.
 
Ni heri wahukumiwe kifungo cha maisha tu.

kama tunafuata utawala wa sheria...basi Wakili wao ana hoja ya msingi kwa mujibu wa vifungu alivyonukuu. Vinginevyo kesi ibadilishwe isiwe ya jinai (sijui kama hili linawezekana)!
 
Jaji ataka upande wa mashtaka usipoteze muda kesi ya Uamsho

Share
bookmark
Print
Email Rating

Baadhi ya viongozi wa Uamsho wakipelekwa mahakamani.
Na Salma Said, Zanzibar (email the author)

Posted Ijumaa,Februari22 2013 saa 10:20 AM
Kwa ufupi
Jaji Mwampashi alimtaka mwendesha mashtaka huyo, kuwasilisha pingamizi hizo wakati ombi hilo litakaposikilizwa hasa kwa kuzingatia kuwa si jipya.
JAJI wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Abraham Mwampashi, anayesikiliza kesi dhidi ya viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu ya Zanzibar (Jumiki), amepinga hoja za upande wa mashtaka za kutaka kutokusikilizwa kwa ombi la upande wa utetezi kuhusu pingamizi ya dhamana.

Jaji Mwampasi alifanya hivyo jana ambapo alisema asingependa kupoteza muda kutokana na mambo ya kiufundi na kwamba kama kuna pingamizi yoyote, ni vizuri Serikali ipange siku ambayo pingamizi hiyo itasikilizwa mahakamani.

Jaji huyo alisema angependa kujua sababu za upande wa mashtaka kutokuwasilisha ombi hilo mapema hasa ikizingatiwa kuwa kesi hiyo imechukua muda mrefu na kwamba kisheria ingeanza kusikilizwa.

Jaji Mwampashi alisema kwa kuwa kuna kesi ya msingi, ni vizuri mahakama ikaendelea kusikiliza ombi hilo badala ya kupoteza muda kwa sababu ya mambo ya kiufundi.

Kwa mujibu wa jaji huyo, upande wa utetezi uliwasilisha ombi hilo tangu mwaka jana.
Mwanasheria kutoka katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, Ramadhan Naseeb, alikiri kuhusu ombi hilo kupokewa tangu mwaka jana.

Jaji Mwampashi alimtaka mwendesha mashtaka huyo, kuwasilisha pingamizi hizo wakati ombi hilo litakaposikilizwa hasa kwa kuzingatia kuwa si jipya.

Hatua hiyo ilikuja baada ya Mwendesha Mashtaka Naseeb, kuiomba Mahakama Kuu, isisikilize ombi la pingamizi la dhamana katika kesi hiyo.

Naseeb alitoa ombi hilo baada ya upande wa utetezi kuwasilisha barua ya kuitaka mahakama ,kufanya mapitio yake kuhusu pingamizi iliyowekwa na upande wa mashtaka ya kuzuia washtakiwa wasipewe dhamana.

Washtakiwa katika kesi huyo ni, Sheikh Farid Hadi Ahmed (41), mkazi wa Mbuyuni, Mselem Ali Mselem (52), mkazi wa Kwamtipura, Mussa Juma (37), mkazi wa Makadara, Azzan Khalid Hamdani (43), mkazi wa Mfenesini, Suleiman Juma, mkazi wa Makadara, Khamis Ali na Hassan Bakari (39), mkazi wa Tomondo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…