Wakili wa Serikali kupiga kura TLS sio haki, ukweli usemwe

Wakili wa Serikali kupiga kura TLS sio haki, ukweli usemwe

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
12,675
Reaction score
25,924
Nimejiuliza sana, mawakili wa serikali wana umoja wao unaitwa TPBA (Tanzania Public Bar Association) yaani umoja wa mawakili wa serikali Tanzania, na wana Rais wao. Upande wetu TLS ukiongea kiuhalisia kabisa, unahusu Mawakili wa kujitegemea.

TLS inajali maslahi ya mawakili wa kujitegemea, na kiuhalisia, mawakili wa serikali na mawakili wa kujitegemea ni vitu viwili tofauti, hata maslahi yao ni tofauti na hata affiliation yake kwa umma dhidi ya Serikali ni tofauti.

Hivi, kweli tuseme wakili wa serikali anayelipwa mshahara na serikali anaweza kupiga kura kinyume na kile Serikali imemtuma unafikiri ni haki? Mtu yeyote mpenda haki na fairness, atakubaliana kwamba hapo hakuna fairness na TLS imeshamezwa.

Mimi ningekuwa ni serikali, ningejiweka kando kabisa na hili jambo, mawakili wa serikali hawatakiwi kupiga kura kwanza hawana leseni ya kufanya kazi kuwakilisha Raia wanawakilisha serikali tu, kwahiyo tuseme TLS ni ya serikali?
Rules zinaweza kuwa zinabada kuwafanya wapige kura lakini fairness na uhalisia, mawakili wa kujitegemea tungeachwa tuchague Rais wetu na tuendeshe mambo yetu kama zilivyo nchi zingine. Ni mawazo yangu tu.
 
Nimejiuliza sana, mawakili wa serikali wana umoja wao unaitwa TPBA (Tanzania Public Bar Association) yaani umoja wa mawakili wa serikali Tanzania, na wana rais wao. upande wetu TLS ukiongea kiuhalisia kabisa, unahusu mawakili wa kujitegemea, TLS inajali maslahi ya mawakili wa kujitegemea, na kiuhalisia, mawakili wa serikali na mawakili wa kujitegemea ni vitu viwili tofauti, hata maslahi yao ni tofauti, na hata affiliation yake kwa umma dhidi ya serikali ni tofauti. Hivi, kweli tuseme wakili wa serikali anayelipwa mshahara na serikali anaweza kupiga kura kinyume na kile serikali imemtuma? unafikiri ni haki? mtu yeyote mpenda haki na fairness, atakubaliana kwamba, hapo hakuna fairness na TLS imeshamezwa.

mimi ningekuwa ni serikali, ningejiweka kando kabisa na hili jambo, mawakili wa serikali hawatakiwi kupiga kura kwanza hawana leseni ya kufanya kazi kuwakilisha raia, wanawakilisha serikali tu, kwahiyo tuseme TLS ni ya serikali? rules zinaweza kuwa zinabada kuwafanya wapige kura lakini fairness na uhalisia, mawakili wa kujitegemea tungeachwa tuchague rais wetu na tuendeshe mambo yetu kama zilivyo nchi zingine. ni mawazo yangu tu.

Ungependa mamba apange mwenyewe kuacha kushambulia watu?

Vipi mhalifu hatimaye kujichagulia adhabu kali kabisa?

Hawa hawawezi kujitoa wenyewe au kuondolewa humo na serikali ndugu!

Hao ni wa kufurushwa, vinginevyo ulichoandika hapa ni kulia lia kule kule kama kwa wale wa katiba mpya.

Viva Gen Z Kenya, Hamas na Palestina na wote wengine popote mliko kwa kulitambua hilo wazi wazi.

Kwa hakika:

"There's no free lunch!"

Alisikika mwuungwana mmoja akijisemea.
 
TLS. ni chama cha wanasheria Tanganyika, sio chama cha mawakili wa kujitegemea
 
Uzi Ufungwe
uzi ukifungwa, nitaamini jf nayo imenunuliwa. ila nawajua, hawawezi kufanya huo upuuzi. kweli wakili wa serikali akapigie kura chama cha mawakili wa kujitegemea?
 
Screenshot_20240731_165127_WhatsApp.jpg
 
Back
Top Bottom