SoC02 Wakinga wanavyorithisha elimu ya uchumi na malezi

SoC02 Wakinga wanavyorithisha elimu ya uchumi na malezi

Stories of Change - 2022 Competition

akyo

Member
Joined
May 6, 2017
Posts
38
Reaction score
25
UTANGULIZI.
Kwanza kabisa,nisemi mimi sio mkinga wala sina vinasaba na wakinga.Ila nimewahi kuishi na wakinga na nimekuwa nikiwauliza masuala mengi.

Kutokana na kukaa nao kuna vitu nimejifunza na ningependa jamii ijifunze.

Kabla sijaeleza vitu nilivyojifunza nitatoa mfano kisha nitaeleza jinsi mambo niliyojifunza kwa jamii hii.

MFANO 1
Mzee mmoja wa kikinga ana watoto 3 wa mke mmoja.Watoto hawa wawili wakiume na wa mwisho ni wakike.

Baba yao ni mfanyabiashara wa vifaa vya kielectronic(Tv,simu, computer n.k). Kabla ya hapo baba yao alikuwa mfanyabiashara wa mazao (mahindi, karanga, maharage).

Baba yao alijitahidi kuwasomesha watoto wote,na Mungu saidia watoto wake walikuwa na uwezo darasani.

Katika udogo wao baba yao alikuwa anawashirikisha kwenye shughuli zake zote, zikiwemo za biashara ya mazao. Pia alikuwa anafundisha umuhimu wa hela na jinsi inavyopatikana.

Mtoto wake wa pili aliwahi nambia "kuna muda nilivyokuwa naenda kumuomba mzee hela ya kula primary, najifikiria kuwa lazima ataanza kunipa maelimu yake ya fedha inavyopatikana kwa ugumu, halafu ndio ananipatia."

Mtoto wake wa Kwanza alifaulu akaenda kusomea udaktari, na kwasasa ni daktari wa binadamu mkoa fulani hapa nchini.

Mtoto wa pili alivyofaulu kwenda kidato cha tano, baba yake alimwambia, nanukuu "Mwanagu ninajua una akili sana, na umefaulu vizuri, ninakuomba tushirikiane kuzisimamia mali hizi, nikufundishe jinsi ya kuziendesha ili nitakapoishiwa nguvu mali hizi zisipotee. Si unajua kaka yako yupo kwenye kazi za watu, dada yako amechagua kusomea uandishi wa habari.

Je unataka tuje kurudi kweye umaskini tena?"

Mtoto wake wa pili anasema aliifikiria sana na siku ya tatu akakubali.

Ninapoandika maandishi leo hii jamaa ana maduka ya kielectronic mawili moja lipo Dar lingine huku mikoani. Kwa sasa wanasaidiana na baba yake,akikwama huyu, huyu anamsaidia, na kwasasa mtoto ndio anaagiza mzigo wa kwake na wa baba yake kutoka nchi za nje.

Nina mifano mingi ya wakinga ambao wamechagua miongoni mwa watoto wao kufanya shughuli anayoifanya yeye.

MAFUNZO NILIYOYAPATA.
•Kufundisha elimu ya fedha kwa watoto wetu, ili mtoto awe anajua kuhifadhi fedha na matumizi mazuri ya fedha.

•Kuchagua angalau mwandelezaji wa mali zako, miongoni mwa wanao ili siku ukiishiwa nguvu/ kufariki mali zisipotee bure.

Zingatia: Lazima ujue na uwaandae watoto ili wasiwe wabinafsi na kujinufaisha wenyewe.

•Kuwashirikisha watoto shughuli zako unazozifanya zinazokuingizia kipato.

•Kupata muda wa kuongea na kuwasikiliza watoto,hii itasaidia kugundua vipaji vyao, changamoto zao.n.k

•Pia ni vizuri kuhimiza ushirikiano kwa watoto kwa kuwapa shughuli zinazotaka ushirikiano.

•Kusikiliza maoni ya watoto,kuhusu hatma yao na ndoto zao.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom