Wako wapi kina Madenge ? mabingwa wa kuitetea CHADEMA kwenye mitandao

Rashda Zunde

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2022
Posts
297
Reaction score
285
Hawa watu ambao kila siku wamekuwa wakijifanya mabingwa wa kuitetea CHADEMA kwenye mitandao—akina Madenge, Sativa, Mwita, Ntobi na wengine—leo wamekosekana kabisa mahakamani kwenye kesi ya Lissu.

Wamekuwa hodari sana kwenye keyboard, wakipiga kelele mtandaoni kana kwamba wao ndio walinzi wa mwisho wa chama. Lakini siku kama ya leo, ambayo ilihitaji uwepo wao wa kweli, si wa maneno, wamekuwa kimya kama hawapo.

Hii inaonyesha wazi kwamba kuna watu wanapenda kutumia matatizo ya wananchi kama chambo la kisiasa, lakini hawako tayari kusimama nao kwenye uhalisia. Wanataka wengine waumie, wao wabaki na “likes” na “retweets.”

Kupiga kelele mitandaoni siyo ujasiri—kuonekana hadharani na kusimama na ukweli ndiyo ujasiri wa kweli.

Msikubali kudanganywa. Hawa watu wanatumia majina yao mitandaoni kuwatumia wananchi kama chambo, lakini wao wenyewe hawako tayari kuchukua hatua hata ya kutokeza mahakamani.

Sasa tunajiuliza: Je, kweli walikuwa wanaitetea CHADEMA au walikuwa wakijitafuta wao wenyewe kwa kutumia jina la chama?
 
Reactions: Lax
Wanapiga pesa za Musk kupitia likes na Comments zenu.
 
ntobi toka lissu aweke nia ya kugombea uenyekiti-- wewe kumuweka hapa kwamba hajatokea kesi ya lissu inakua kama utani...

hoja ya kwamba watu wengi wanasupport movement online kuliko kwa ground hapa nchini-- majibu yapo clear hayahitaji hata common sense
 
Umemsahau Onesmo Mushi bingwa wa kutweet X akimshambulia Mbowe.
 
Reactions: Lax
Wanasubiri Oktoba wazuie uchaguzi kutokea mtandaoni.
 
Vijana wa aina Yako wanasafari ndefu sana ya kufikia Tanzania ambayo serikali Yako ya Ccm imekuwa ikiimba kama sala ya Baba yetu Since uhuru komaa huku huku jf Kuna wenzio watakuunga mkono tofauti na X (Twitter)
 

Attachments

  • Screenshot_20250424-170444.jpg
    371.5 KB · Views: 31
Reactions: Lax
Wapiga soga tu hao hapa kuna Salary slip...
 
saa ya ukombozi imekaribia!

#NoReformsNoElection
 
Vijana wa aina Yako wanasafari ndefu sana ya kufikia Tanzania ambayo serikali Yako ya Ccm imekuwa ikiimba kama sala ya Baba yetu Since uhuru komaa huku huku jf Kuna wenzio watakuunga mkono tofauti na X (Twitter)
Unamaanisha?????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…