gemmanuel265
JF-Expert Member
- Feb 16, 2016
- 8,485
- 18,048
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu, hawa viongozi wa serikali walioruhusu mabilioni ya Tegeta Escrow Account kutolewa Bank Kuu (BOT) kwanini hawajaunganishwa kwenye kesi ya jinai ya uhujumu uchumi inayowakabili James Rugemalila na mwenzie Harbinder Singh Seth, ikiwa wao kama viongozi wa serikali ndio walioruhusu mabilioni hayo kutolewa?!
Tukiangalia mtiririko wa viongozi wa serikali waliopaswa kuwa sehemu ya watuhumiwa wa kesi ya jinai ya uhujumu uchumi wa bilioni 306 za Tegeta Escrow Account zilizokuwa Banki Kuu ni pamoja na:
1. Gavana wa Benki Kuu
2. Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
3. Waziri wa Fedha
4. Paymaster General
5. Rais wa nchi (ili mabilioni yale yatoke BOT ni lazima rais aruhusu malipo hayo)
Wapo pia wale waliothibitisha kupokea mgawo wa malipo hayo haramu (wao walisema walipewa kama zawadi sababu ya ukaribu wao na James Rugemalila) kama:
1. Andrew Chenge (mb)
2. Anna Kajumlo Tibaijuka (mb)
3. William Ngeleja (mb)
4. Shabaan Ngurumo (mtumishi wa Ikulu ya utawala wa awamu ya 4)
5. Majaji
6. Maaskofu na Mapadre
Hapa lazima tuhoji inakuwaje waliokamatwa ni wafanyabiashara tu waliochotewa mabilioni hayo lakini Mawaziri pamoja na maafisa wa serikali walioruhusu mabilioni hayo kutoka, au na wale waliopata mgawo wa hayo mabilioni kama zawadi wakiendelea kula mema ya nchi bila hofu yoyote?!
Namkumbusha pia rais wangu Magufuli asisahau kuwashughulikia wale wote waliofanya ufisadi wa kivuko kibovu cha Bagamoyo kilichogharimu ma billions of money ya walalahoi wa nchi hii kilichoishia kwenda rout moja tu ya Bagamoyo wakati wa uzinduzi iliyoambatana na mbwembwe nyingi zenye tambo kibao za kisiasa kwa Waziri aliyehusika na Wizara hiyo kwa kipindi hicho, tofauti na hapo hakijawahi kuonekana tena kilikofichwa.