Wako wapi wachezaji hawa wa soka letu?

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2023
Posts
1,483
Reaction score
2,392
Wanamichezo nawasabahi.Kwa wale wapenda Michezo hasa Mpira wa Miguu wa miaka ile SIO hawa wa 2000 naomba kujua Walipo wachezaji hawa na Wanajishughulisha na Shughuli/biashara gani baada ya KUSTAAFU SOKA.
1. Aluu Ally-mchezaji wa Simba
2. Malota Soma-Simba
3. Yanga Bwanga-Yanga
4. Zamoyoni Mogella-Simba
5. Nteze John_Simba
6. Mohamed Tostao-Yanga
7. Idd Seleman-Simba
8. Jella Mtagwa
9. Mtemi Ramadhani-Simba
10. Idelfonce Mwamlima-Yanga

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Malota Soma ni dereva wa teksi Magomeni,Idd Selemani "Mayor" amefariki,Ntenze John ni mchungaji ambaye makazi yake ni nchini Marekani akiihubiri Injili,Jellah Mtagwa yuko nyumbani kwake Magomeni Kagera akiendelea kujiuguza na maradhi,Idelfonce Amlima yuko nyumbani kwao Mtwara akijishughulisha na biashara binafsi
 
Asante sana kwa taarifa Pole nyingi kwa familia ya Marehemu Idd Seleman Mungu ampe pumziko stahiki na wengine wenye taarifa za wachezaji wetu wa zamani tujulishane ili tuonekane kuwaenzi kwa michango yao

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…