Jana Jioni Baada ya Kuchoshwa na Kazi za Kaisari, niliingia You tube kutafuta nyimbo nilizokuwa nikizisikiliza.
Nikabahatika kumkumbuka Msanii mmoja toka Iringa akifahamika kama Mike T aka Mnyalu. Kwa haraka nikazikumbuka kazi zake mbili KAMA na NYALU LAND.
Kisha nikamkumbuka Babu Inspekta Haruni na kazi yake ya BINTI KISURA.
Nilijikuta natabasamu muda wote. Hakika wasanii hawa walibarikiwa; nyimbo zina mashairi matamu hasa, zina muwala unaoeleweka.
Napenda kujua wako wapi na wanafanya nini sasa?