Bonde la Baraka
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 4,580
- 7,943
Habari wanabodi!
Nimeona niliweke sawa jambo hili lililohusu ukoloni Tanzania (Tanganyika) kuanzia utawala wa Kijerumani miaka ya 1880's- 1918 baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia na kisha utawala wa Mwingereza ulioanza mwaka 1919-1961 (wakati wa uhuru)
Kwa hakika watu huchanganya mafaili mawili, faili la enzi za utunwa na lile linalozungumzia ukoloni.
Enzi za ukoloni East Afrika, Tanganyika ikiwemo wakoloni/wazungu walitawala kwa misingi ya haki za binadamu, huku wakifuata sheria walizozitunga.
Yapo madhaifu madogomadogo yaliyojitokeza katika utawala wao ila hayakuwa makubwa sana, walihesabu nchi kama mali yao.
Kikwazo kikubwa kwa wananchi kilikuwa kodi za kichwa ambazo hata nchi mama kama Uingereza na Ujerumani kwa kipindi hicho ilikuwa ikitozwa kama kawaida; tena kwa kiasi kikubwa kidogo zaidi ya kile kilichotozwa kwa Watanganyika.
Waafrika wachache walioelimika waliwatumia Waafrika wenzao( non- educated persons) kuwashawishi hata wamwage damu zao kuung'oa utawala wa Kizungu ili wao washike nafasi za uongozi.
Nimeongea na vikongwe kadhaa kuwadadisi ikiwa kulikuwa na manyanyaso ya dhahiri kutoka kwa wakoloni wengi walishindwa kuniambia zaidi ya kodi ya kichwa ambayo ilikuwa fedha ya kiasi ambayo kila mtu huweza kuipata kwa wakati huo.