Wakongwe, mashabiki wawatetea chipukizi waliokosa penati England

Wakongwe, mashabiki wawatetea chipukizi waliokosa penati England

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Wakati mashabiki wakiwatuliza wachezaji chipukizi waliopoteza penati zao na kusababisha England ishindwe kuondoa nuksi ya miaka 55 ya ukame wa vikombe, Gary Naville amemtaka winga wa Arsenal, Bukayo Saka kutembea kichwa juu licha ya kushindwa kufunga penati muhimu ya tano dhidi ya Italia.

Saka, Jadon Sancho na Marcus Rashford walishindwa kuingiza wavuni mikwaju yao ya penati dhidi ya Italia baada ya mechi hiyo ya fainali ya Mataifa ya Ulaya, Euro 2020, kuisha kwa sare ya bao 1-1 katika muda wa kawaida na nyongeza na Italia kufanikiwa kutumbukiza penati tatu huku England ikipata mbili tu kupitia kwa Harry Maguire na Harry Kane.

England ilianza kwa kasi na kutangulia kupata bao mapema katika sekunde ya 57 wakati Luke Shaw alipopiga kiki iliyompita kipa Gianluigi Donnarumma, likiwa ni bao lililofungwa mapema zaidi katika fainali za Ulaya.

Lakini katikati ya kipindi cha pili, Leonardo Bonucci aliisawazishia Italia alipousukumia mpira wavuni kumpita kipa Jordan Pickford, kabla ya mechi hiyo kuamuliwa kwa penati.

"Ni dhahiri ni kitu kinachoumiza kwa mvulana huyu (Saka). Enzi za kulaumu wapiga penati kwa kushindwa kufunga, zimeisha," tovuti ya HITC imemkariri Neville, beki wa zamani wa Manchester United na timu ya taifa ya England baada ya Saka kushindwa kumfunga kipa wa Italia, Gianluigi Donnarumma kwenye Uwanja wa Wembley.

“Kila mtu amempenda kijana huyi kwa wiki chache zilizopita, pia watampenda kwa wiki chache zijazo. Amekuwa akifanya vizuri.
“Huyu kijana, asiinamishe kichwa kwa sababu tutamlinda kwa miezi michache ijayo.”

Saka, ambaye ana miaka 19, pia alitetewa na kocha wake Gareth Southgate, akisema yeye kama mwalimu ndiye anayetakiwa kubeba lawama.

Saka, ambaye aliachwa katika mechi ya nusu fainali dhidi ya Denmark, jana Jumapili aliingizwa uwanjani muda mfupi baada ya Mtaliano Bonucci kusawazisha bao la kuongoza la England, na akawa tishio kwa ngome ya Italia.

Lakini aliangua kilio mara baada ya kipa Mtaliano kuokoa mkwaju wake wa penati na wachezaji wenzake walionekana wakimfariji uwanjani.

"Ni suala langu. Niliamua wapiga penati kwa kuzingatia tulichofanya mazoezini, na hakuna aliyejiamulia,’ Southgate aliiambia BBC Sport katika mahojiano baada ya mechi.

"Tumeshinda pamoja ni suala letu wote kwa kutoweza kushinda mechi usiku huu, lakini kwa kuangalia penati, huo ni uamuzi wangu na nawajibika kikamilifu.

"Tulikuwa tumejiandaa vizuri na tulianza vizuri. Lakini bahati mbaya wachezaji hawakuweza kumalizia leo. "Hawawezi kujiangalia kwa jinsi walivyofanya mazoezi, wasingeweza kufanya zaidi au vizuri zaidi."

Mbali na Saka, Rashford na Sancho, ambao muda mfupi ujao watakuwa klabu moja, waliingizwa mwishoni mwa mchezo lakini wakshindwa kutumia penati zao vizuri.
 
Southgate ndo chanzo kikubwa cha mattizo ya England tokea mwanzo wa michuano,,,ni kana kwamba anaendekeza chuki fulani kwa wachezaj fulani na kuwabeba wengine mfano mzuri ni chuki za wazi alizoonesha kwa Grealish na Henderson ni dhairi kwamba hakuwa nao vizur mpaka kupelekea kutowapanga na kuwa anawatoa toa ovyo.

Hata baada ya kuwaingiza, jana kama aliona tatizo la kufunga Sterling alimuacha wa nini wakati dhairi alikua anaonesha kuchoka na kushinda hata kucheza mpira ukwel wa mambo ni kwamba mafanikio ya England yatakuja wakiacha personal interest na hate kwa makundi ya watu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom