JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, ameutumia ujumbe wake wakati wa misa ya mkesha wa Pasaka kulaani kile amekitaja ukatili wa vita unaoshuhudiwa nchini Ukraine.
Bila kuitaja moja kwa moja Urusi, Baba Mtakatifu ametoa wito wa kuwepo usitishaji mapigano katika siku ya leo ya Pasaka kwa malengo ya kufikia makubaliano ya amani kwa njia ya mazungumzo.
Sikukuu ya Pasaka, ambayo ni miongoni sherehe muhimu katika kalenda ya dini ya Kikristo, husherehekewa kila mwaka kwa waumini kuhudhuria misa, kuandaa karamu na wengine kutembeleana.
Source: DW