Wakristo duniani washerehea sikukuu ya Pasaka, Papa alaani ‘ukatili’ Nchini Ukraine

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mamilioni ya waumini wa dini ya Kikristo duniani leo Aprili 17, 2022 wanasherehekea Sikukuu ya Pasaka kukumbuka kufufuka kwa Yesu Kristo baada ya kusulubiwa msalabani zaidi ya miaka 2000 iliyopita.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, ameutumia ujumbe wake wakati wa misa ya mkesha wa Pasaka kulaani kile amekitaja ukatili wa vita unaoshuhudiwa nchini Ukraine.

Bila kuitaja moja kwa moja Urusi, Baba Mtakatifu ametoa wito wa kuwepo usitishaji mapigano katika siku ya leo ya Pasaka kwa malengo ya kufikia makubaliano ya amani kwa njia ya mazungumzo.

Sikukuu ya Pasaka, ambayo ni miongoni sherehe muhimu katika kalenda ya dini ya Kikristo, husherehekewa kila mwaka kwa waumini kuhudhuria misa, kuandaa karamu na wengine kutembeleana.


Source: DW
 
Wala sadaka wa dunia nawaona na majoho yao.
 
Papa kaa kwa kutulia
 
Lakini si tumekubaliana Russia anachapika kule Ukraine??

Sent from my Redmi Note 9S using JamiiForums mobile app
Hata yeye anapata taarifa zinazopingana. Hivyo anashjndwa kujua anayepigwa ni nani na nani anapiga. Ndo maana kaishia kulaani mauaji kule ukrein. Kwakuwa hajui nani anapiga nani anapigwa

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…