kaka umeomba programs zipi? Kaka mimi pia nina hali kama yako,na ilinibidi nikae mwaka mzima nyumbani,kwa kukosa ada ya chuo. Katika kipindi chote nilichokaa nyumbani,nilijifunza kwamba mtoto wa maskini hachagui. Mwaka huu nilifanya applcations kwa kulenga programs zenye kipaumbele cha mkopo(education). Pia niliomba na diploma ya ualimu(nimepangiwa korogwe). Hii inamaanisha kwamba,nikikosa mkopo,naenda kusoma diploma,nikipata namshukuru mungu. Nakushauri,kama hukuomba programs zenye kipaumbele cha mkopo,nenda chuo chochote cha serikali kinachotoa diploma ya ualimu,ueleze matatizo yako na uombe nafasi ya kwenda kusoma ualimu. Ndoto zako utazitimiza baadae,naomba uamini ninayokuambia.