DOKEZO Wakufunzi SAUT - Mwanza baadhi wananyanyasa na kufelisha wanafunzi makusudi

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Chuo cha SAUT kina wakufunzi baadhi wananyanyasa sana wanafunzi, wanawafelisha makusudi na bado hata wanafunzi wakirudia mitihani hawawajazii kwa kudai wao wako busy hawawezi kushughulikia wanafunzi wanaorudia somo

Kuna mkufunzi wa shule ya Sheria amewafelisha na kuwashikilia wanafunzi wengi tangu Mwaka wao wa kwanza katika somo lake la Constitutional Law mpaka mwaka wa 3 na wengine kabisa mpaka mwaka wa nne na ni tabia pia ya walimu wengi wa SAUT kushikilia kwa kusudi wanafunzi

Wapo walimu waadilifu mno na wanawasaidia sana wanafunzi kufanikiwa ila baadhi ni wanyanyaji, wananyanyasa pia mabinti kingono wakiwataka kimapenzi ila wakiwakataa wanawafelisha mpaka watakapowakubali

Wakufunzi wengine wanafikia hatua ya kufelisha hadi group members na marafiki wanaowaona na hao mabinti hadi watakapowakubali na wanaweka wazi kuwa hawawezi kufaulu hadi wawakubali

Hii inadhoofisha sana taaluma za wengi na kukatisha tamaa wengi, inarudisha nyuma sana maendeleo maana tunatengeneza taifa lenye vijana wenye visasi na walevi wa madaraka wakiamini kwa madaraka yao wanaweza kupata na kufanya lolote lile walitakalo.

Waajiri wa wakufunzi wa vyuo waangalie pia historia na maadili ya wanaotaka kuwaajiri maana kuajiri kwa kigezo cha kufaulu sana ama kujua sana somo sio jambo muhimu ila muhimu ni kuangalia maslahi ya wanafunzi na taifa kwa ujumla.
 
Hapo SAUT nimesoma
Hayo mambo yapo
Yaani mkufunzi kuonekana ni mzuri hadi afelishe wanafunzi wengi, ndo anaheshimika na uongozi
Nadhani ingekuwa vizuri hawa wakufunzi kuwasaidia wanafunzi kufaulu na wakufelisha uongozi wa chuo uchunguze.
SAUT alipotoka Kitima mambo yanaharibika
Lakini wakatoliki ni watu makini nadhani wafanyie kazi hizi tuhuma
 
Kuna mwalimu kamaliza degree yake hapo akapata nafasi ya kufundisha chuo cha kati cha afya alichokuwa anafanyia hapo kakihamishia huku anapofanyia kazi sasa hivi bila fedha huboi CA lazima ufeli tu....itakuwa aliiga
 
Ndio maana kila siku nawaambia msijistress kulipa mamilioni kwenye shule za English Mediums. Haya sasa twende kazi, watoe watoto wako shule ya EM wapeleke Kayumba haraka sana.

Thank me later

🙏🏻🙏🏻🙏🏻🙏🏻
 
Hilo jambo liangaliwe kwa pande zote. Kama kuna wakufunzi wenye hizo tabia, wadhibitiwe mapema ili wasiiharibu taswira ya chuo.

Lakini kama na nyinyi wanachuo pia kama mnazembea kwenye masomo yenu, muongeze bidii. Maana nyinyi utandawazi haujawaacha salama! Na pia hamjawahi kuwa malaika.
 
Chuo cha SAUT kina wakufunzi baadhi wananyanyasa sana wanafunzi, wanawafelisha makusudi na bado hata wanafunzi wakirudia mitihani hawawajazii kwa kudai wao wako busy hawawezi kushughulikia wanafunzi wanaorudia somo

Kuna mkufunzi wa shule ya Sheria amewafelisha na kuwashikilia wanafunzi wengi tangu Mwaka wao wa kwanza katika somo lake la Constitutional Law mpaka mwaka wa 3 na wengine kabisa mpaka mwaka wa nne na ni tabia pia ya walimu wengi wa SAUT kushikilia kwa kusudi wanafunzi

Wapo walimu waadilifu mno na wanawasaidia sana wanafunzi kufanikiwa ila baadhi ni wanyanyaji, wananyanyasa pia mabinti kingono wakiwataka kimapenzi ila wakiwakataa wanawafelisha mpaka watakapowakubali

Wakufunzi wengine wanafikia hatua ya kufelisha hadi group members na marafiki wanaowaona na hao mabinti hadi watakapowakubali na wanaweka wazi kuwa hawawezi kufaulu hadi wawakubali

Hii inadhoofisha sana taaluma za wengi na kukatisha tamaa wengi, inarudisha nyuma sana maendeleo maana tunatengeneza taifa lenye vijana wenye visasi na walevi wa madaraka wakiamini kwa madaraka yao wanaweza kupata na kufanya lolote lile walitakalo.

Waajiri wa wakufunzi wa vyuo waangalie pia historia na maadili ya wanaotaka kuwaajiri maana kuajiri kwa kigezo cha kufaulu sana ama kujua sana somo sio jambo muhimu ila muhimu ni kuangalia maslahi ya wanafunzi na taifa kwa ujumla.
These allegations is for all universities. has never resolved!
 
Back
Top Bottom