molwe
JF-Expert Member
- Jan 10, 2015
- 416
- 440
Habari za leo wanajamvi!! Wakulima wa mpunga dakawa-Morogoro, Wana kilio!! Wafugaji wanaingiza mifugo mashambani kwa jeuri, wakulima hawana cha kufanya!! Ukikamata ng'ombe upeleke polisi, mwenyewe hatokei wanasubiri giza wanawaswaga na kuondoka nao.
Kuna kipindi kwa ustaarabu kabisaa walikaa kikao Cha wakulima na wafugaji na kukubaliana kuwa hakuna kuingiza mifugo mashambani hadi wakulima wavune, na ni kuanzia mwezi wa 8 tarehe 30
Sasa Cha ajabu tangu wakulima wanapanda wanakimbizana na ng'ombe hadi wanavuna!! Tunaomba msaada kama kuna wahusika humu mtusaidie, maana wafugaji wana silaha lakini wakulima hawana