Wakulima India wabomoa minara 1500 ya simu

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Maandamano ya wakulima yanayoendelea nchini India hasa hasa jimbo la Punjab yamepelekea minara ya simu ipatayo 1500 kuharibiwa. Uharibifu huo ni kwa kuiba majenereta yanayoendesha mitambo hiyo na kukatwa kwa nyaya za mawasiliano zinazoiunganisha na minara mingine.
Katika moja ya video iliyosambazwa mitandao wakulima hao wameoneshwa wakiwafurusha wafanyakazi wa moja ya minara hiyo.Maandamano ya wakulima yamekuwa yakiendelea kwa zaidi ya mwezi sasa tangu pale waziri mkuu wa nchi hiyo Narenda Modi kutia saini sheria mpya ya kilimo mnamo mwezi Septemba ambapo wakulima hao wameona sheria hiyo ipo dhidi ya maslahi yao.
Wakulima wamebaini sheria hiyo mpya itayafaidisha zaidi makampuni makubwa yakiwemo yale ya mitandao ya simu.Makampuni yaliyotajwa kuelekea kuwanyonya wakulima ni pamoja na Reliance inayomiliki biashara ya mawasilano na Adani inayojishughulisha zaidi na kilimo cha kibiashara.
1609226065959.png
 
View attachment 1662023
Nawaunga mkono wakulima wenzangu.
 
Back
Top Bottom