Wakulima kanda ya kaskazini wahofia njaa baada ya kupata mavuno haba

Wakulima kanda ya kaskazini wahofia njaa baada ya kupata mavuno haba

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
9,140
Reaction score
15,963
Wakulima kanda ya kaskazini wahofia njaa baada ya kupata mavuno hafifu kwa kile wanachodai mvua kukata mapema mwaka huu.

Baadhi ya wakulima kutoka katika mikoa ya kilimanjaro ,manyara wamesema ni kweli mvua zilikuwa nyingi sana mwaka huu LakinI pia ziliwahi kukata kabla ya mazao Kufikia stage nzuri.

Mmoja katI ya wakulima waliokosa mazao amesema yeye Amelima heka tatu za mahindi Lakin amevuna magunia matano tu ya Mahindi.,

Na mkulima mwingine aliyelima nusu heka ameishia kupata madebe matatu ya mahindi tu na hivyo kufanya wahisi Dalili ya njaa mwakani.

Wakulima hao wameelezea kuPata hasara kubwa kutokana Gharama walizotumia tangu maandalizi ya shamba,kulima, kununua mbegu kupalilia,mbolea ,nk.
 
Poleni serikali sikivu ya mama itawaletea chakula cha msaada
 
Nusu heka debe 3 alichelewa ama hakupanda mbegu Bora, nimepanda kajisehemu cha nje ambapo hata ¼kg ya mahindi haikuisha ila nimepata hizo debe 3 tena na hapo nishachoma
 
Back
Top Bottom