Wakulima Mbeya walia uhaba mbolea ya ruzuku

Wakulima Mbeya walia uhaba mbolea ya ruzuku

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Wakulima wa Tarafa ya Kiwanja, Halmashauri ya Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya wamelalamikia uhaba wa mbolea na pembejeo za ruzuku.

Wakizungumza haya Novemba 28, 2022 wakati wakizungumza na mwandishi wa habari hizi ambapo wamedai kuwa katika maeneo yao mpaka sasa hakuna mawakala wa pembejeo licha ya wao kuandaa mashamba yao mapema.

Mkazi wa maeneo ya Chunya, Daniel Mwantengule ni mkulima anasema wakulima bado hawajui ni wapi watapata pembejeo za kilimo kama mbolea na mbegu kwani wanasikia wilaya zingine tayari mbolea za ruzuku zilishafika lakini kwa Wilaya ya Chunya ni kimya na baadhi ya maeneo wameanza kupanda mazao.

"Tuliambiwa kuwa pembejeo zitaanza kufika mwezi Agosti lakini mpaka sasa kimya na maeneo tunayoishi hakuna mawakala wa mbolea ya ruzuku na hatujui hatima yetu,” amesema Mwantengule."

Mkulima Mwingine Joylene Ruben, Kata ya Mbugani anasema hali ya upatikanaji wa mbolea za ruzuku bado ni changamoto kutokana na mbolea hizo kutofika mpaka sasa. Hivyo, ameomba serikali iweze kuliona hilo ili wakulima wasiingie gharama kubwa kama msimu uliopita.

Amesema msimu wa kilimo ulioisha mwaka 2022 tulikumbana na bei kubwa ya pembejeo za kilimo ambazo zilipelekea baadhi ya wananchi wasio na fedha kushindwa kulima kutokana na bei ya mbolea kuwa juu ambapo tulikuwa tukinunua mbolea mfuko mmoja wa Dap ilifika mpaka Sh100,000 mbolea ya urea ilikuwa Sh70,000.

Kwa upande wake afisa kilimo na umwagiliaji Wilaya ya Chunya, Cuthbert Mwinuka amekiri kuwepo kwa changamoto ya uhaba wa mawakala wa kuuza mbolea za ruzuku Tarafa ya kiwanja Wilaya ya Chunya mbapo amesema mpaka sasa mawakala waliopo kwa wilaya nzima ni wawili tu, ambao wapo Kata ya Chalangwa na mwingine yupo Kata ya Makongolosi.

Mwinuka amesema ameeleza kuwa uchache wa mawakala unatokana na mawakala kushindwa kutimiza masharti ya serikali yaliyowekwa. Serikali imeomba wakulima wawe na subira wakati inaendelea na mazungumzo na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa ili waweze kuleta mbolea na wakulima pia wanufaike na ruzuku hizo.

Aidha Mwinuka amefafanua kuwa Wilaya ya Chunya ina tarafa mbili na wakulima waliosajiliwaa ni zaidi ya elfu 20,000.

Tarafa hizo ni kiwanja na tarafa na tarafa ya Kipembawe lakini tarafa tarafa yenye Changamtoto ya upatikanaji wa pembejeo ni tarafa ya kiwanja ambapo hakuna kilimo cha tumbaku kwani kwenye Tarafa ya Kipembawe walishafikishiwa pembejeo za kilimo pamoja na mbolea
 
Back
Top Bottom