nyamwingi
JF-Expert Member
- Mar 10, 2016
- 944
- 872
Katika utafiti nilioufanya leo hii tar. 24.02.2022 Bei za mbolea zimepanda Mara dufu lakin kwa bahati mbaya serikali hadi sasa ipo kimya huku ikijua wazi kuwa Ruvuma-Songea ndio mikoa inayozalisha kwa wingi zao la mahindi kiasi Cha kuweza kusaidia Tanzania kuwa na akiba ya chakula. Leo Bei za mbolea za kuzalishia zimefikia Kama ifuatavyo:
1. CAN-86,000(pia hapatikani)
2. SA-70,000 kutoka 64,500 siku wiki moja nyuma
3. NPK-91,500
Kwa bei hizi za mwaka huu zinawasababishia wakulima wa mkoa wa Ruvuma kutumia mbolea za asili ili angalau kupoza maumivu ya gharama.
Kama waziri wa kilimo ndgu Hussein Bashe yupo nchini hajaambatana na MH. Rais wetu mpendwa Samia Suluhu Hassan basi kuna haja ya kuchukua hatua za dharuru za haraka katika kuhakikisha Bei ya mbolea ziwe rafiki kwa mkulima hali itayopelekea nchi kuwa na utulivu wa chakula cha kutosha.