Wakulima wa Alizeti walalamikia kuuziwa Alizeti feki ya Ruzuku

VYEMELO

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2020
Posts
349
Reaction score
464
Ujumbe huu ni maalum kwa Waziri wa Kilimo na Chakula, mheshimiwa Bashe. Awali ya yote nikupongeze kwa juhudi na kazi kubwa na nzuri unayofanya ktk kuiongoza Wizara hii nyeti.

Wakulima tunaziona jitihada zako na maono uliyonayo ya kukitoa kilimo hapa kilipo na kukipeleka hatua ya juu zaidi. Lakini pia, wakulima wadogo tunakushukuru kwa namna unavyoonesha nia ya kutusaidia na kutujali. Tunashuhudia kupitia vyombo mbalimbali vya habari namna unavyopigana kuhakikisha uzalishaji wetu unakuwa na tija kubwa kupitia upatikanaji wa pembejeo, masoko ya mazao, mitaji ya kuwawezesha wakulima kuendeshea shughuli zao za shamba, na kadhalika. Tunakushukuru na hongera sana Mheshimiwa Hussein Mohamed Bashe.

Hata hivyo, nina Neno juu yako. Neno hili Naamini linawawakilisha wakulima wengi Nchini pia. Kwa maneno mengine, Ni kilio cha wananchi. Vilio vya wakulima, hususan wakulima wadogo (Smallholder farmers), juu ya Wizara yako ni vingi;

Hapa nitataja vichache tu.

Serikali tangu uhuru, imekuwa ikifanya jitihada kubwa kuwawezesha wakulima kuzalisha kwa tija kwa kuhakikisha huduma za ugani (Agro-Extension services), pembejeo za kilimo, vifaa vya kulimia, Hifadhi ya mazao, masoko, sera, na kadhalika, vinamfikia mkulima. Changamoto ni watendaji ktk Wizara yako; hasa watendaji walio ktk ngazi ya huko Wizarani. Most of them are corrupt. Kuwa makini nao.

NAMBA 1:
Nchi imekuwa ktk hali ya upungufu mkubwa wa mafuta ya kula kwa miaka mitatu sasa. Upungufu huu umesababisha bei ya mafuta ya kula kuwa juu. Kwa mfano, lita moja ya mafuta ya alizeti huku mikoa ya Nyanda za juu kusini imeuzwa hadi shilingi 10,000/=! Bei hii ni kubwa sana ikilinganishwa na kipato kidogo cha watu kwa siku, mwezi, na hata mwaka.

Serikali ktk kukabiliana na changamoto hii ilichukuwa hatua za makusudi msimu wa kilimo wa 2021/2022 kutoa ruzuku kwenye mbegu ya Alizeti (mbegu bora) na kuisambaza kwa wakulima ambao kwa kweli tulilipia labda gharama za usafirishaji pekee; kwa sababu, tulitoa shilingi 3,500/= kwa mbegu ya kupanda ekari moja! Ikilinganishwa na shilingi 45,000/= tunayonunulia mbegu aina kama Hysum 33. Wakulima tulifurahi Kwelikweli na tuliishukuru na kuipongeza Serikali. Tulinunua kwa wingi mbegu hiyo na kupanda kwa maelekezo yote ya Maafisa ugani-kilimo.

Mheshimiwa, mbegu iliota; ilipoanza kukua sasa; Ilipoanza kutoa maua; Maua yalipoweka mbegu sasa; kuchunguza mbegu (maana sisi ni wakulima wa siku nyingi. Tuna uzoefu mkubwa na Alizeti), tulikuwa tumepanda alizeti aina zaidi ya nne (varieties)! Kuna yenye mbegu nyeusi, yenye mbegu nyeupe, kahawia, michirizi myeupe na myeusi; kuna ndefu zaidi ya mita tatu na haiweki maua, kuna ndefu inayoweka suckers nyingi hata zaidi ya sita zenye maua yasiyo na mbegu. Na kadhalika.

Kimbembe kingine, alizeti hiyo ni 'mapepe'. Haina kile kiini cha mafuta ndani yake. Binafsi nimekamua kwenye mashine ya Kichina ya kisasa kabisa, Gunia moja (kilo 60) limetoa lita 7 za mafuta! Kwa kawaida, alizeti nzuri iliyotokana na mbegu bora za kisasa hutoa lita 18 hadi 22 za mafuta.

Mheshimiwa usichukie wala usichoke kusoma hii. Itakusaidia. Unajua hawa Watendaji wako wa Kilimo wanachofanya inapotokea fursa ya Serikali kuweka Ruzuku kwenye mambo mbalimbali ya kumsaidia mkulima Nchini? Ngoja nikutonye! Walichofanya; walikwenda kuchukuwa alizeti wanakojua (aidha, ile inayouzwa sokoni bila kujali ni ya aina gani, kisha wakaifungasha kwenye vifungashio vizuri; au, kama ilichukuliwa kutoka kwa vituo vya uzalishaji mbegu, zilichukuliwa zile za hovyo na kuzifungasha, na, "wanaume" wakavuta mamilioni yaliyotolewa na Serikali wakaweka mifukoni!

Haya tuliyashuhudia hata miaka ile ya 2010s Serikali ilipoweka Ruzuku kwenye mbegu za mahindi. Wataalam hawa wa kilimo kwa kushirikiana na mawakala wa pembejeo za kilimo wasio waaminifu, walikuwa wanakwenda vijijini wananunua gunia moja (kilo 100) kwa 15,000/=. Wanachambua na kubaki na kilo 80, wana-pack kwenye vifungashio. Wanasambaza kwa wakulima kwa bei ya 3,000/= kwa kilo. Hebu piga hesabu mafisadi hao walivyokuwa wanapata Super profit. Kwa gunia moja alikuwa analipwa na Serikali 240,000/=; ukitoa 15,000/= na gharama nyingine, anabaki na faida ya almost 200,000/= kwa kila gunia! Kilimo hakiwezi kuendelea mbele kwa mtindo huu. Serikali haiwezi kufanikiwa kumkwamua mkulima.

Mheshimiwa, wakulima wanalia alizeti hii. Fuatilia ili uwajibishe watu!

NAMBA 2:

Serikali imebaini kuwa mojawapo ya changamoto inayowatesa wakulima ni upungufu mkubwa wa mitaji ya kuendeshea shughuli za shamba. Katika hili ilichukuwa hatua ya kuzungumza na mabenki ya biashara na Mifuko mbalimbali ya Serikali (e g. Mfuko wa Pembejeo) kutengeneza mazingira mazuri yatakayowezesha wakulima kukopesheka. Tunashukuru juhudi za Rais, Mama Samia Suluhu Hassan pamoja Nawe Waziri Bashe kwa hili. Taasisi hizi za kifedha zilikubali hata zikashusha interest rate (IR) kutoka digit 2 hadi 1, na, zilirekebisha na masharti mengine mengi na kuwa nafuu kulingana na hali ya sisi wakulima wadogo.

Kimbembe, nenda kaombe mkopo huko! Lugha utakayokutana nayo kutoka kwa hawa Watendaji! Unajiuliza, hivi nani mkubwa ktk Nchi hii? Mbona wote ni 'kambale'. Wote wana sharubu! Nchi inakosa Chain of Command ati!
Mheshimiwa Rais kaagiza, Waziri kaweka msisitizo, kaagiza; Utekelezaji wa hovyo! Watendaji hawatii maagizo ya wakubwa wao. Unajiuliza, hivi Rais na Waziri wake wanatuzuga wakulima kuturidhisha kwa malengo ya kisiasa?
Unajiuliza; hivi hizi pesa mabilioni Serikali imesema imeziweka kwenye mabenki ya biashara pamoja na Mifuko ili wakulima wakakope huko kukuza mitaji ya kilimo, zimewekwa kweli? Kama zimewekwa, zinapotelea wapi na kwa nani?
Kuna wachumi wa mitaani wanasema, ...

Ni michongo ya 'wakubwa', wanatengeneza Mpango na kuwatangazia wananchi, pesa zinaingizwa huko, wakulima wachache wanapatiwa (tena kwa kutoa 'chochote'!) na baadaye 'wakubwa' hawa wanakwenda kuzichota. Nchi haiwezi kuendeshwa namna hii. Njia ya mtu muongo Ni fupi. Unaweza kuwadanganya watu mara nyingi, lakini kamwe,huwezi kuwadanganya siku zote.

Waziri Bashe, nina mashaka makubwa hata juu ya Utekelezaji kwa mafanikio Mpango wa Ruzuku ya Pembejeo za Kilimo ulioutengeneza na wataalam wako huko Wizarani. Hautofanikiwa. Watendaji huko Wizarani hutengeneza Mpango ulio na nyufa zitakazowawezesha kufanya ufisadi. Anyway, hukuwepo kwenye system wakati wa Utekelezaji wa Mpango wa Pembejeo za Ruzuku kipindi cha Serikali ya awamu ya Nne na Tano. Ni majanga!

Serikali, tuoneeni huruma wakulima wadogo. Tusaidieni. Kilimo kikiwezeshwa kutakuwa na tija kubwa. Kitavuta vijana kuingia shambani na kuzalisha. Umaskini utatoweka. Watanzania tutakuwa na maisha bora. Serikali ya Chama Cha Mapinduzi itaimarika na kudumu.

Muwe mnakuja na huku chini vijijini kwa wakulima na kutushirikisha ktk mipango ya kuendeleza. Haiyumkiniki, wakulima tunaweza kuwa tunakielewa kilimo kuliko ninyi wasomi. Kilimo ndiyo maisha yetu. Tushirikiane. Mnapanga mipango itakayowanufaisha ninyi. Siyo vema hivyo. Tutosheke na mishahara yetu. Mbona "Mama" kawaongezea ninyi Watumishi wa umma mishahara na posho?!

Kwani Mungu aliwapangia ninyi tuu kuwa na maisha mazuri hapa Duniani? Kilimo kimekuwa kama kazi ya laana. Nimewahi kuwasikia baadhi ya viongozi wetu wanapowaadabishe watumishi walio chini yao, ... Nitakufukuza kazi Uende ukalime huko maporini! Huu ni mtizamo potofu juu ya kilimo na wakulima. Mbona mkistaafu mnatafuta mashamba na mifugo? Mnakuja kwetu wakulima? Ndugu zangu, kwa Tanzania, kilimo ndiyo ajira, kilimo ndiyo maisha. Tusikibeze wala kuwadharau wakulima. Mbona 90% ya chakula mnachokula enyi Watendaji wa Serikali tunakizalisha sisi Wakulima wadogo?

Mheshimiwa Hussein Mohamed Bashe, mambo ya kusema kuhusu Wizara ya Kilimo na Chakula ni mengi, itoshe kwa haya mawili. Tupo pamoja nawe kukupasha taarifa ninazoamini zitakusaidia ktk kuisimamia barabara Wizara complicated kuliko unavyoweza kuwaza. Najua wanakudharau kwa background yako, elimu yako, na kadhalika. Watendaji wa kilimo hasa ktk ngazi ya Wizara wako stubborn mno. Hujiona wamesoma sana na ati wanajua mambo yote. Hawaambiliki. Hawashauriki. Kidogo ungekuwa hata na MSc. Agriculture wangekuheshimu, Au PhD ktk fani ya kilimo. Wako very stubborn and corrupt. Waangalie sana Mheshimiwa wasije wakakuharibia destiny yako.

Ubarikiwe Mheshimiwa Hussein Mohamed Bashe!
 
Huu ujumbe ndio nauona baada ya kutumia mbegu feki za ASA za alizeti. Yaani full mapepe
 
Naona ya mbolea ya Minjingu yakijirudia. Haya ndo madhara ya kukimbiza kuingiza mbegu sokoni bila tafti za kutosha.
 
Back
Top Bottom