Ighombe
JF-Expert Member
- Feb 12, 2014
- 1,181
- 675
Habari wadau wa Jf,
Mhe. Diwani wa kata ya Kilomeni Wilaya ya Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro ameagiza Miche 34,000 kutoka kituo cha utafiti wa Kilimo Lyamungo kwa lengo la kufufua Kilimo hicho! Kilimo cha buni aina ya Arabica kilishamiri mkoani hapa miaka ya 90 kurudi nyuma.
Hata hivyo kilikabiliwa na changamoto ya kuporomoka kwa bei ya kahawa katika solo LA Dunia. Shime vijana waendeshaji boda boda na wengine wenye changamoto ya ajira kutokea Kilomeni tujikite kwenye Kilimo hicho.
Mhe. pia ameagiza wataalam kutoka Njombe nyanda za juu kusini kukagua eneo hilo na kutoa ushauri ikiwa Kilimo cha Parachichi kinafaa eneo hilo.
Wamehakikishia kuwa hali ya hewa inaruhusu.