Wakulima wa korosho bado hawajamaliza kulipwa, msimu mpya umeanza korosho bei ni TZS 2,556

Wakulima wa korosho bado hawajamaliza kulipwa, msimu mpya umeanza korosho bei ni TZS 2,556

The Assassin

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2018
Posts
4,942
Reaction score
20,077
Nimeona tweet ya Naibu Waziri wa Kilimo Mheshimiwa Bashe akisema wakulima wa korosho wa mwaka jana ambao serikali ilichukua korosho zao bado wanaendelea kulipwa, nimeshangaa siyo kidogo.

Mwaka mzima serikali inalipa nini? Hayo malipo yasiyoisha ni malipo ya namna gani? Mtu aliuza korosho zake toka mwaka jana hadi leo hajalipwa? Juzi nimesikia Mheshimiwa Rais akisema walipwe haraka, ila mbona malipo yamechukua muda mrefu sana?

Serikali waoneeni huruma wakulima wa korosho.

20191101_080216.jpg

Hiyo bei isikutishe Mkuu kumbuka kuwa hiyo ni siku ya Kwanza ya mnada hata mwaka juzi msimu wa 2017-2018 bei ya mnada wa Kwanza ilikuwa tsh 1580/= lakini baada ya wiki kadhaa mbele korosho iliuzwa Kwa tsh 3000/=(msimu ambao mbuzi walinyweshwa soda na bia)

Ngoja tusubiri tuone itakuaje huko mbele
 
Hua inapanda tu ila sio kushuka mkuu?
 
Back
Top Bottom