DOKEZO Wakulima wa Korosho wa Mkunya Wilaya ya Newala hatujalipwa zaidi ya miezi miwili, wengine wamelipwa pungufu ya makubaliano

DOKEZO Wakulima wa Korosho wa Mkunya Wilaya ya Newala hatujalipwa zaidi ya miezi miwili, wengine wamelipwa pungufu ya makubaliano

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

NBica

Member
Joined
Sep 13, 2010
Posts
39
Reaction score
36
Sisi Wakulima wa Korosho tuliopo Mkunya Wilayani Newala Mkoani Mtwara tulipimishwa korosho tangu Oktoba na wengine Novemba 2024, hapo nikiwa namaanisha wale maafisa wa Serikali walikamilisha taratibu zote za manunuzi wakaondoka na mzigo kwa ahadi kuwa tutalipwa muda sio mrefu.

Kwa kawaida hela huwa inatoka ndani ya wiki mbili mara baada ya mchakato kama huo kufanyika lakini sasa hivi huu unaenda mwezi wa tatu sasa, kila siku danadana, hakuna majibu ya kueleweka kutoka Serikalini.

Wakati wa mchakato wa manunuzi tulikubaliana kuwa gharama ya kilo moja ya korosho ni Shilingi 3,000 lakini muda ulivyopita na wakulima kuanza kulalamika baadhi yetu wakaanza kuingiziwa malipo ambayo kimahesabu yalionesha wamelipwa Sh 2,200 kwa kilo.

Wale waliolipwa walipoona malipo yaliyoingizwa kwenye akaunti ni pungufu ndipo wakahoji kwa wale Maafisa wa Serikali waliopo Ghala Kuu ambao hata hawakusema kuwa malipo yatakuwa pungufu, ndio wakajibu kwa kusema eti kuna unyaufu wa korosho.

Sasa huo unyaufu unatoka wapi wakati mwanzoni tulikubaliana kila kitu kuwa kipo sawa na hadi bei tukapanga pamoja!

Matukio kama hayo huwa yanatokea mara kwa mara, tunachotaka kujua ni kweli hiyo hela iliyolipwa ni kweli imetoka hivyo Serikali Kuu au kuna watu wamecheza nayo hapo Katikati na mbona hawakutoa maelezo mapema?

Tunaomba Serikali pamoja na Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) watupe majibu ya kinachoendelea, je, ni kweli kuna unayufu wa korosho tulizowauzia? Mbona hawakusema awali? Mbona haikuwa hivyo wakati wa makubaliano ya mauzo na je sisi ambao hatujalipwa ‘status’ yetu ipoje?

Kuna wenzetu Wakulima wa Korosho katika Chama Kikuu cha Ushirika TANECU (Tandahimba & Newala cooprative Union) nao wanalia kama sisi

Tumehangaika kutafuta viongozi hususan Waziri mwenye dhamana lakini naye yupo kimya, Mkuu wa Wilaya anajua yupo kimya. Afisa Ushirika nae yupo kimya. kuna harufu isiyo ya kawaida. Tunaomba utupazie sauti tunaenda mwezi wa pili sasa tangu korosho zetu ziuzwe na hatujalipwa.

Wanachelewesha makusudi ili walipe bei pungufu ya ile waliyouza mizigo huo, maana ni madili ya watu haya na wakulima hawana pa kusemea.
 
Changamoto ya malipo ya korosho mkoa wa Mtwara inakera sana jamani hadi sas wakulima hawajalipwaa elaa za mnada wa 8,9 ambaoo tangu mwez wa 11 mnada ulipitaa
 
Sa100 na serikali yakr hana huruma na watanganyika hususani wakazi wa mikoa ya kusini...shida na nyie watu wakusini wajinga sana,mana ndio shamba la kura la ccm..ikataeni ccm waziwazi.
 
Mamcu wametoa tangazo wanafunga maimu kama hamjalipwa kuanzia mnada wa 1-10 fikeni ofis ya karibu.

Bila shaka hata Tanecu inawahusu
 
Shida si kwa serikali, shida ipo huko kwenye vyama vyenu vya ushirika!! Mnachaguana kwa kujuana sana hata kwa nafasi zonazohitaji wasomi!! Mnawekana ndugu tupu na Wala rushwa.

Utakuta fungu limeshatoka muda mrefu muhasibu anaanza kuishenyeta hela yenu!! Matumizi ya kutanua tuu na starehe!! Hajali lolote maana kunawatu anakula nao.

Shida sio serikali shida ni hao wahasibu wenu uchwara wasio na elimu ndo muwachunguze
 
Back
Top Bottom