Mgombea wa nafasi ya Rais wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewahakikishia wakulima wa Tumbaku nchini kuwa Serikali iko kwenye hatua za mwisho kuhakikisha madai yao ya muda mrefu yanalipwa.
Dkt. Samia amesema jitihada za serikali kupitia Wizara ya Kilimo zinaendelea kuhakikisha kampuni mbili zinazodaiwa fedha za wakulima zinalipa stahiki hizo.
"Niwapongeze na niwashukuru wakulima wa Tumbaku… mmeongeza uzalishaji na Tanzania sasa inauza Tumbaku kwa kiasi kikubwa, kwahiyo niwapongeze sana, na lile suala la mikopo na wakulima kuchelewa kupewa fedha zao halipo tena, niwapongeze sana "Dkt.Samia Suluhu Hassan -Mgombea Urais CCM.