Wakulima wadogo wote watageuka vibarua kwenye mashamba ya hawa mabepari

kabila01

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2009
Posts
4,235
Reaction score
4,964
Habari wna bodi

Wiki iliyopita nilikua na ziara yangu binafsi katika baadhi ya vijiji vya mkoa wa Iringa. Nimejionea mashamba makubwa ya mahindi yanamwagiliwa kwa mitambo. Kwa sasa wenyeji wanasubiri mvua ndo walime wale wawekezaji mahindi yao yaanaanza kuchanua. Kwa hali hii ikiendelea miaka mitatu ijayo tutakua na haya
1. wakulima wadogo wote watageuka vibarua kwenye mashamba ya hawa mabepari maana hawatakua na uwezo wa kulima katika mashamba yao kutokana na bei kubwa hizi za mbolea
2. Hakutakua na mkulima mdogo bali wote tutategemea kununua unga kutoka kwa hawa mabepari wenye mashamba makubwa
3. Tutakua tunafanya vibarua kwenye haya mashamba kwa kunyanyaswa na kipato kidogo tutakachopata kitaishia kununua chakula( Tunageuka watumwa kwenye ardhi zetu)
 
Kwahiyo unataka tubaki na kilimo cha kizamani?

Au kuna katazo la wakulima wadogo kujiongeza?

Hao wakubwa wamefikiaje ukubwa

Nadhani badala ya kulalama ungeulizaw ni nini kinafanyika kuwajenga peasants ili nao wawe wakulima wakubwa
 
Siioni mwelekeo wa serikali katika kuwasaidia wakulima wadogo kufika huko. Kwa bei hizi za mbolea na serkali kukaa kimya inaonyesha ndo mpango wa kibepari kuelekea huko
 
Habari wna bodi

Wiki iliyopita nilikua na ziara yangu binafsi katika baadhi ya vijiji vya mkoa wa Iringa. Nimejionea mashamba makubwa ya mahindi yanamwagiliwa kwa mitambo. Kwa sasa wenyeji wanasubiri mvua ndo walime wale wawekezaji mahindi yao yaanaanza kuchanua. Kwa hali hii ikiendelea miaka mitatu ijayo tutakua na haya
1. wakulima wadogo wote watageuka vibarua kwenye mashamba ya hawa mabepari maana hawatakua na uwezo wa kulima katika mashamba yao kutokana na bei kubwa hizi za mbolea
2. Hakutakua na mkulima mdogo bali wote tutategemea kununua unga kutoka kwa hawa mabepari wenye mashamba makubwa
3. Tutakua tunafanya vibarua kwenye haya mashamba kwa kunyanyaswa na kipato kidogo tutakachopata kitaishia kununua chakula( Tunageuka watumwa kwenye ardhi zetu)
Mkuu ni maeneo gani au Kijiji gani nami nipite angalau nijifunze kitu
 
Mkijiunga hata wakulima 3 hadi 4 wataweza kulima kwa umwagiliaji na kumudu gharama za mbolea. Pump ya umwagiliaji na mipira yake hiifiki laki 4.
 
Unadhani nazungumzia vipump hivi ya diesel hawa wanatumia mitambo ambayo ndani ya saa moja inamwagia ekari 100
 
Mkijiunga hata wakulima 3 hadi 4 wataweza kulima kwa umwagiliaji na kumudu gharama za mbolea. Pump ya umwagiliaji na mipira yake hiifiki laki 4.
Hahaha mkuu kwa utani ama una maanisha, hao wakulima wa 4 hata wajimwambafy vp hawawezi mudu gharama za pembejeo(mbolea) kwa msimu huu sasa zana za kilimo wataweza kweli
 
Hilo mbona lipo wazi katika sekta zote...., In the world of Competition na A Big Fish eating a Smaller Fish its just a matter of time.....

Kumbuka pia competition ninyaoongelea zio internal peke yake (ndani ya nchi) bali na nje ya nchi..., Na with current system ya wasionacho wataachwa kwa spidi ya mwanga.., Hopefully hata hizo ajira kwenye hayo mashamba zitapatikana sababu with machinery nani anahitaji binadamu msumbufu anayeumwa, kuomba likizo na kulalamika......
 
Mkijiunga hata wakulima 3 hadi 4 wataweza kulima kwa umwagiliaji na kumudu gharama za mbolea. Pump ya umwagiliaji na mipira yake hiifiki laki 4.
Alafu kwa gharama ya hizo mbolea na mazao yakiiva bei isipokuwa rafiki kama mwaka jana mahindi wajitutumue wanunue wenyewe na kula wenyewe ?
 
Hahaha mkuu kwa utani ama una maanisha, hao wakulima wa 4 hata wajimwambafy vp hawawezi mudu gharama za pembejeo(mbolea) kwa msimu huu sasa zana za kilimo wataweza kweli
Wanaanza kidogo kidogo watafanikiwa.
 
Usilalamike kuhusu hao wawekezaji au mabepari kama unavyowaita

Miaka yote hiyo hiyo ardhi ipo na wameshindwa kuitumia hata kwa mikopo
Anakuja muwekezaji kapewa ardhi kihalali na kaingiza hela ndefu uje uanze kumlaani tena

Mimi naona na viboko mchapwe wakati mnamwagilia mashamba yao na hakuna kupumzika siku nzima
Kama tumeshindwa kujiendeleza wenyewe kwanini tumtafute mchawi

Mimi natoa 10m I swear kama kutapatikana watu wengine wa kufanya mradi kama huo
Tusikalie maneno tu bali tunaweza pia

Na kama tutalaumu tu mwisho wa siku hao hao wataanza kuiba mahindi ya muwekezaji na mwisho atafunga virago na kurudi kwao
Hilo ndio tunajua zaidi
 
Back
Top Bottom