Wakurugenzi wa Halmashauri Jengeni Vituo vya Bodaboda: Mhe. Mchengerwa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

WAKURUGENZI WA HALMASHAURI JENGENI VITUO VYA BODABODA - MHE. MCHENGERWA

Waziri wa Nchi, OR-TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuhakikisha wanajenga vituo vya bodaboda vya kupaki pikipiki vyenye uwezo wa kuzuia jua na kuwakinga na mvua wanaposubiri wateja.

Mhe. Mchengerwa ametoa maelekezo hayo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salam, wakati akizindua sare maalum (uniform) na mfumo wa kidijitali (kanzidata) wa madereva Bodaboda na bajaji wa jiji la Dar es Salaam.

“Ninaelekeza vituo hivi vijengwe mara moja ili kuwasaidia bodaboda kupata eneo salama la kupaki wakati wakisubiria wateja,” Mhe. Mchengerwa amesisitiza.

Mhe. Mchengerwa amewahimiza Wakuu wa Mikoa nchini nchi nzima kusimamia uandaaji wa mfumo wa kidijitali (kanzidata) wa kuwatambua madereva Bodaboda na bajaji kama ilivyofanyika katika mkoa wa Dar es Salaam.

Aidha, Mhe. Mchengerwa amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya nchini kuwalinda na kuwathamini maafisa usafirishaji hao maarufu kama madereva bodaboda na bajaji, kama ambavyo Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza.

Sanjari na hilo, Mhe. Mchengerwa amewaelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuweka utaratibu utakaowawezesha maafisa usafirishaji hao kunufaika na mikopo ya asilimia 10 ya halmashauri ambao unawalenga wanawake, vijana na wenye ulemavu.

“Wakurugenzi wa halmashauri wekeni utaratibu mahususi utakaowawezesha maafisa usafirishaji kunufaika na mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri zenu kwa kundi la wanawake, vijana na wenye ulemavu,” Mhe. Mchengerwa amehimiza.

Waziri Mchengerwa ameelekeza mchakato wa kutoa mikopo ya asilimia 10 uanze mara moja ndani ya mwezi huu wa Julai, 2024 ili walengwa wanufaike na mikopo hiyo kama ilivyokusudiwa na Serikali ya Awamu ya Sita.
 
Attachments

  • GRdRj2XWcAAEyse.jpg
    GRdRj2XWcAAEyse.jpg
    324.6 KB · Views: 3
  • GRdRj2gXsAApqtM.jpg
    GRdRj2gXsAApqtM.jpg
    372.7 KB · Views: 3
  • GRdRj24aoAAEJcv.jpg
    GRdRj24aoAAEJcv.jpg
    756.1 KB · Views: 3
  • GRdRj2OWYAADPzZ.jpg
    GRdRj2OWYAADPzZ.jpg
    443.8 KB · Views: 3
  • Thanks
Reactions: Y2J
Nchi ya ajabu sana hii yani baada serikali ije na mpango jinsi gani itapunguza ongezeko la vijana kuwa boda boda inakuja na mbinu ya kuongeza boda boda yani kuongeza kundi la umaskini Tanzania
 
WAKURUGENZI WA HALMASHAURI JENGENI VITUO VYA BODABODA - MHE. MCHENGERWA

Waziri wa Nchi, OR-TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuhakikisha wanajenga vituo vya bodaboda vya kupaki pikipiki vyenye uwezo wa kuzuia jua na kuwakinga na mvua wanaposubiri wateja.

Mhe. Mchengerwa ametoa maelekezo hayo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salam, wakati akizindua sare maalum (uniform) na mfumo wa kidijitali (kanzidata) wa madereva Bodaboda na bajaji wa jiji la Dar es Salaam.

“Ninaelekeza vituo hivi vijengwe mara moja ili kuwasaidia bodaboda kupata eneo salama la kupaki wakati wakisubiria wateja,” Mhe. Mchengerwa amesisitiza.

Mhe. Mchengerwa amewahimiza Wakuu wa Mikoa nchini nchi nzima kusimamia uandaaji wa mfumo wa kidijitali (kanzidata) wa kuwatambua madereva Bodaboda na bajaji kama ilivyofanyika katika mkoa wa Dar es Salaam.

Aidha, Mhe. Mchengerwa amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya nchini kuwalinda na kuwathamini maafisa usafirishaji hao maarufu kama madereva bodaboda na bajaji, kama ambavyo Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza.

Sanjari na hilo, Mhe. Mchengerwa amewaelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuweka utaratibu utakaowawezesha maafisa usafirishaji hao kunufaika na mikopo ya asilimia 10 ya halmashauri ambao unawalenga wanawake, vijana na wenye ulemavu.

“Wakurugenzi wa halmashauri wekeni utaratibu mahususi utakaowawezesha maafisa usafirishaji kunufaika na mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri zenu kwa kundi la wanawake, vijana na wenye ulemavu,” Mhe. Mchengerwa amehimiza.

Waziri Mchengerwa ameelekeza mchakato wa kutoa mikopo ya asilimia 10 uanze mara moja ndani ya mwezi huu wa Julai, 2024 ili walengwa wanufaike na mikopo hiyo kama ilivyokusudiwa na Serikali ya Awamu ya sita.
Mwaka wa kushiba...
 
Nchi ya ajabu sana hii yani baada serikali ije na mpango jinsi gani itapunguza ongezeko la vijana kuwa boda boda inakuja na mbinu ya kuongeza boda boda yani kuongeza kundi la umaskini Tanzania
Hujui unalosema mkuu kwa taarifa yako bodaboda wanawapita watumishi kibao vipato
 
Nionyeshe boda boda kumi wenye nyumba za kisasa wenye usafiri wa kutembelea na wanasomesha watoto private school na chuo kikuu na miye nikuletee hao watumishi unaosema wanazidiwa kipato na boda boda

Buku buku za kila siku zisikuchanganye kijana umri unaenda hutoweza endesha boda na maisha yana badirika stuka
 
Masikini ni daraja la wanasiasa
 
Nchi ya ajabu sana hii yani baada serikali ije na mpango jinsi gani itapunguza ongezeko la vijana kuwa boda boda inakuja na mbinu ya kuongeza boda boda yani kuongeza kundi la umaskini Tanzania
Toa mawazo yako siyo kulalamika halafu usichukulie negative kila linalofanywa na serikali
 
tunalalamika ila wenye jukumu la kutunga sera wajue tunawastukia mambo wanayofanya maana wanajua kabisa bodaboda siyo kazi kwani inamadhara kiafya pia kipato chake si cha kubadilisha maisha ni kupata pesa ya kula tu je unaitaji Taifa la watu wanaotafuta pesa ya kula tu
 
Back
Top Bottom