MtoMsimbazi
JF-Expert Member
- Aug 19, 2009
- 1,800
- 3,091
Kwa hali ya kushangaza nilimtembea rafiki yangu maeneo ya Ubungo Kibangu, wakati tunapiga story tukasikia mtu anagonga mlango, rafiki yangu wa muda mrefu tangu tupo A-level akafungua mlango ili atambue nani anabisha, alipofungua alikuwa mama wa makamo akiwa anakusanya hela za kuzolea taka, chakushangaza alimwambia atoe elfu 3, akaanza kuhoji kwakuwa yule rafiki hana familia wala hakuna anaeshinda mle kwenye chumba chake, na huwa hapiki kabisa hivyo hata taka zenyewe hazalishi na chumba chake ni self, ilifikia hatua alikataa kutoa kabisa mpka apate maelezo lkn yule mama alikataa akasema mpk apewe elfu 3 yake ndio aondoke.
Jamaa kwa kuepusha usumbufu akaona isiwe shida akampatia na kuondoka, ila hii hali si ya kawaida kwakweli haiwezekani nyumba yenye vyumba 7 na wote bachela mama anakusanya elfu 3 yake, na mbaya zaidi baada ya kupeleleza hawazifikishi kunakohusika kwakuwa kisheria wanatakiwa kukusanya hela kwa kila nyumba na kila chumba, imefikia sehemu inakuwa kero kwakuwa siku za Jumapili au mapumziko wanakuja saa 12 asubuhi kugonga milango wakiwa wanafuatilia kumbe hizo hela wanapiga huku wananchi wakiwa na barabara mbovu za mitaani kuzunguka maeneo mengi barabara zinakuwa makorogoi mvua ikinyesha na baada ya muda wanapitisha greda halafu habari imekwisha.
Tangu kipindi cha kabla chadema hawalichukua jimbo, wakapita na sasa limerudi ccm, wanachojivunia na ile barabara moja ya lami aliohimiza marehemu mhe. JPM, barabara nyingine ni makorogo tupu mvua zikinyesha.WEZI KWELI KWELI