Wakusanya tozo za parking Jijini Mwanza wala Rushwa wakubwa mtaa wa Kalutta

Wakusanya tozo za parking Jijini Mwanza wala Rushwa wakubwa mtaa wa Kalutta

tripof

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2024
Posts
829
Reaction score
1,120
Mkurugenzi wa jiji kuna kikundi kinachotoza tozo za parking jijini Mwanza hususani eneo la mtaa wa Kaluta wanakamata magari na kuyafunga minyororo huku wakidai Rushwa msipoangalia kikundi hiki kitawaharibia kabisa CCM kipindi hiki kwa vile wanafai kutumwa kufanya hivyo na Mkurugenzi Kibamba, siyo watu wazuri kikundi hicho kivujwe au kipewe mafunzo ya customer service waache kutisha watu na kuchukua hongo.
 
Mkurugenzi wa jiji kuna kikundi kinachotoza tozo za parking jijini Mwanza hususani eneo la mtaa wa Kaluta wanakamata magari na kuyafunga minyororo huku wakidai Rushwa msipoangalia kikundi hiki kitawaharibia kabisa CCM kipindi hiki kwa vile wanafai kutumwa kufanya hivyo na Mkurugenzi Kibamba,siyo watu wazuri kikundi hicho kivujwe au kipewe mafunzo ya customer service waache kutisha watu na kuchukua hongo.
Sijui Watanzania huwa mahitaji yetu ni yapi? Hao majambazi yanayopora pesa za watu kwa nguvu kisa umepaki gari vibaya mnayahusisha na CCM, jenga hoja ili matatizo yafanyiwe kazi na viongozi maana uwezo wa kuitoa CCM madarakani haupo kabisa kwa hiyo inabidi tuishi nao na turekebishe pale panapotakiwa kurekebishwa.
 
Yaani badala ya parking fee jero unaombwa rushwa ya shilingi ngapi?
CCM umeingiaje?

Hebu lipeni bhana, hizi zingine ni aibu kulialia.
 
Wengine wanaomba mia tano wasikuandikie Buku ya parking
 
Hiki ni kikundi kibaya sana. Waliwahi kunifunga mnyororo wakidai niwalipe 50,000. Nikawaomba control number hawana. Wezi kabisa.
 
Back
Top Bottom