Wakuu Kwa Hizi Mashine za Kuatamisha Kuku, JN8-48

Wakuu Kwa Hizi Mashine za Kuatamisha Kuku, JN8-48

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2011
Posts
7,872
Reaction score
9,263
Wakuu kama kuna anaye hitaji hizi Mashine basi tuwasiliane, ni Made in China ila zina Ubora mzuri sana katika kutotoresha Mayai na unaweza totoresha mayai ya Kuku, Kanga, Bata, na Hata Ndege

Feature zake

1. Ni Automatic, means inageza Mayai yenyewe, ina contro joto na ina alamu ya kukualifu kama Joto au Humidity imezidi au kupungua kiwango kinacho takiwa

2. Haina kelele, Iko kimya

3. Inaweza Fanya kazi muda mrefu

4. Uwezo wa kutotoa ni 96%

5. Ina saa ya kukuwezesha kuseti ni muda unao taka igeuze mayai: Mfano unaweza seti ikawa inageuza kila baada ya masaa 5

6. Nguvu zake
- 100W
-110V , 220- 240 V

7. Vitu kama Joto na Humudity inayo takiwa vinategemeana na sehemu uliko, Mfano Dar au sehemu zenye Baridi kama Mbeya, hutofautiana

20101026153941742.jpg

Ukijaribu kutazma kwa umakini utaona kuna sehemu ya Kuhesabu Siku ambazo uliweka Mayai, Masaa, Humidity% na joto C, na kwa juu kabisa kuna Air Vent kati kati ya hayo matundu makubwa
57241_208227_F.jpg

$(KGrHqJHJDoE8fkjbuKIBPNc3DD(4Q~~60_35.JPG

POOZOO04.jpg

Muenakano wake kwa Ndani, Tray yake inabeba mayai ya saizi zote, na Hicho kidude Cheupe ndo kifaa ya kugeuzia mayai

Bei yake ni Tsh 450,000/

Unaweza ni Call kwnye hii namba 0783691072


KATIKA MATUMIZI YA HIZI INCUBATORS KUNA MAMBO Y KUZINGATIA

1, Eneo ulipo wewe mfano sehemu zenye Joto au Baridi kari

3. Mayai unayo tumia

3. Kuhakikisha maji hayaishi kwenye mashine make yakiisha tu mayai yata kauka

4. Kugeza mayai ndani ya siku ya 1-18

5. Kuhakikisha kiwango cha Humidity na Joto ziko sawa






 
Umeme wa tanesco ukikatika inakuaje?

Mkuu kwa Consuption yake ukiwa na Solar ta W 15O na Inventor ya W hata 300 unakua umemaliza kazi inaweza washa kazi 24 hours yaani kwa hii solar na Inventor unaweza kabisa usitumie umeme wa TANESCO, ila kwa backup unakuwa ni chini ya hapo
 
Mkuu inauwezo wa kubeba mayai kiasi gani???

Maana nikihesabu hapo kwenye tray naona kama 48 tu au nimekosea????
 
Mkuu inauwezo wa kubeba mayai kiasi gani???

Maana nikihesabu hapo kwenye tray naona kama 48 tu au nimekosea????

Yapu JN8-48 Inabeba mayai 48 ila ukitaka kubwa maana yake ni za aina tofauti, ila kwa hii model ni kiwango hicho tu, ukizidi hapo inakuwa ni model ya mfano wa Jokofu, Ila hata yenyewe ukitaka utapata
 
Yapu JN8-48 Inabeba mayai 48 ila ukitaka kubwa maana yake ni za aina tofauti, ila kwa hii model ni kiwango hicho tu, ukizidi hapo inakuwa ni model ya mfano wa Jokofu, Ila hata yenyewe ukitaka utapata

hii ndogo sana kibiashara haina maslahi. Vipi hizo kubwa zina uwezo gani na bei yake. Angalau yakuanzia mayai 500 mpaka 1000
 
hii ndogo sana kibiashara haina maslahi. Vipi hizo kubwa zina uwezo gani na bei yake. Angalau yakuanzia mayai 500 mpaka 1000

Mkuu hazilipi kivipi? Kila kitu huanza Chini, ni lazima uanzie chini, ili kusoma mazingira ya biashara na baada ya hpo unapo kuwa umetengeneza mtandao mzuri na umepostion vizuri ndo unapanua biashara na hapo unkuwa tiyali unamtaji na soko la uhakika na si la kusimuliwa tu kwamba kuna wateja kumbe hakuna,

Ya kubw zinapatikana na nawea kukuunganisha na jamaa wa huko China kama ukiwa tiyali.
 
Mayai yanakaa siku ngapi humo hadi kifaranga kitokee?

Contacts zako?
 
Mayai yanakaa siku ngapi humo hadi kifaranga kitokee?

Contacts zako?

Mkuu kibiolojia ni siku 21 kwa sabababu kwenye hizi mashine kinacho fanywa ni sawa na anacho fanya kuku, Ila unawza ukaamua kuharakisha mayai yatotorewe mapema inawezekana, ila hao kuku/vifaranga hawatakua na afya nzuri watakuwa dhaifu

Na huenda hata baadhi ya makampuni ya vifaranga huwa wanafanya mchezo huo, ndo maana some time unakuta vifaranga wa kampuni fulani wanakuwa dhaifu na wanaugua sana au kufa kwa wingi
 
Chasha,Umeme ukikatika inakuwaje na Mayai ndio kwishne?


Mkuu unaweza tumia solar kama Back-up, Ila ukiwa na solar kubwa na invetor ya W kwenye 200 au 300 unaweza usitumie kabisa Umeme make itakuwa na uwezo wa kuendesha Mashine kwa 21 day zote bila tatizo lolote lile, nazani watalaamu wa umeme wanajua hilo,

Ila hata hivyo kama ni umeme wa kukatika masaa mawili au matatu haiona shida bado joto linalo kuwepo lina uwezo wa kuhumili kwa masaa 5, Tatizo ni pale umeme utakapo katika halafu tatizo labda ni Nguzo au watu wameiba mafuta ya Transforma,

Ila mkuu Umeme haupaswi kuwa kikwazo cha wewe kufanya biashara, ukiwa kama Mjasirimali vile vile ni lazima utumie kukatika kwa umeme kama Furusa fulani na si kama kero,

Ila jamaa wanazo kubwa zinazo tumia Gesi kama Back-up, ila ukianza kutumia geii maana yake ni lazima hata mayai uanze kugeuza kwa mkono, kwa sababu gesi huwa ni kutoa joto tu, na ili mayai yageuzwe na mashine ni lazima kuwepo na umeme,
 
Aina za Incubators? Ukiachilia mbali souce of power, Kiutalamu kuna Aina kuu mbili za Incubators

1. Forced Air Incubators

Hii huwa nafeni kwa ndani na hiyo feni husaidia kutawanya joto kwenye mayai, na uzuri wa Forced Air incubators ni kwamba hata Joto ikizidi haitaharibu mayai kwa sababu feni inasaidia kupunguza hilo joto,

2. Still- Air Incubators

Hii haina feni, na inategemea Contro za Nje, so kwa hii aina ni lazima mtu awe karibu na mashine 24 hour ili kucheki, lakini kwa ile aina ya kwanza ukiwa na uhakika na umeme na ukawa umeongeza maji ya kutosha kwenye mashine unakuwa hauna haja ya kuwepo muda wote


Hizi ndo aina kuu za Incubators na unapo enda kununua incubator hakikisha unajua hili, make mara nyingi katika ununuzi wa Incubators unatakiwa kutambua hiyo aina na vilevile kutambua kama incubators in Automatic au Manual
 
Back
Top Bottom