Tajiri.
Ushauri tu, ukitaka Mazda Axela aka Mazda3 nunua kuanzia ya mwaka 2014 kuja juu.
Kuna mabadiriko makubwa mawili Mazda alifanya.
1. Aliacha kutumia Ford chasis, na kuamua kuja na platform yake. Walishare na Ford nyingi ikiwemo Ford Focus.
2. Aliintroduce engine yake binafsi inayotumia technology ya SkyActiv.
Kwanini nashauri utafute kuanzia hii 3rd generation?
1. Ford chasis ilikua na changamoto kubwa sana ya kutu.
2. SkyActiv engine (diesel au petrol) zina ulaji mzuri sana wa mafuta.
3. Muonekano wa 3rd generation mbele nyuma na ndani ni mzuri sana (ingawa uzuri wa kitu ni machoni mwa mtazamaji).
Naongelea muonekano ambao Mazda wanauita Kodo design, ulioanza kwenye CX5 ukaja kwenye Atenza na mtu wa tatu ku-adopt akawa Axela.
4. Una option nyingi za displacement kuanzia cc 1500 hadi 2500, either Diesel au Petrol.
5. Hazipishani sana gharama na 2nd generation.