Wakuu msaada perfume

Wakuu msaada perfume

G_real

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2019
Posts
684
Reaction score
855
wakuu nahitaji perfume au bodyspray nzuri ya bei rahisi kikwapa kinanitesa saana msaada wenu
 
Sijawahi kusoma kokote kidaktari kuwa perfume ni dawa ya kikwapa. Tatua tatizo na usifiche tatizo kwenye mgongo wa manukato
ndo unielekeze mkuu naweza kutatuaje
 
Kama linasumbua sana nenda hospitali utapewa matibabu sahihi..mfano antibiotics..maana kuna vikwapa sio vya kawaida i.e inakuwa ni ugonjwa (Bromidrosis)

Perfume inamask tu harufu mbaya ya kwapa na haitibu tatizo
 
Anza na hii deodorant (POWER HOUSE) ni 2,500-3,000 kabla ya kurukia perfume,ukisha kuwa vizuri ongezea na perfume na hizo Body spray unazozitaka,ukihitaji ushauri zaidi njoo PM...
 
Kama linasumbua sana nenda hospitali utapewa matibabu sahihi..mfano antibiotics..maana kuna vikwapa sio vya kawaida i.e inakuwa ni ugonjwa (Bromidrosis)
Perfume inamask tu harufu mbaya ya kwapa na haitibu tatizo
asante mkuu ndafanya ivyo
 
ndo unielekeze mkuu naweza kutatuaje
Baadhi ya hatua za awali za kufuata.

Usafi wa kwapa lenyewe
Usafi wa nguo unazo vaa ukiziangalia zimeacha unjano sehemu ambapo kwapa linakuwa? Kama ndio hata ufue kwa namna gani huo unjano hauwes kuisha kirahisi na ukiivaa tena lazima kwapa linuke. Mbadala? Uchome nguo? Hapana zichemshie maji ya mto zitie humo au kafulie kwenye mashine za kufulia.
je wajua mazoez yatakayo kufanya utokwe jasho yanaweza kukupunguzia au kuondoa tatua tatizo hilo?
Kwa sababu ukifanya hivyo baadae ukiwa umetulia au hata upo na pilikapilika ndogondogo hata ukitokwa jasho halitakuwa la kunuka.
KAMA MAZOEZI NA HILO SWALA LA KUZICHEMSHA NGUO NDANI YA MAJI YA MOTO LITAKUSHINDA na kama tatizo

ni bakteria... nenda duka la dawa lolte lililo karibu nawe katafute dawa iliyopo kwenye tube zinazotibu vibarango mba wa ngozi n,k nunua mara nyingi bei huanzia 5000 kushuka chini ukimaliza kuoga hasa nyakat za usiku pakaa kesho asubuh oga vaa shati lako sepa kwenye mishe zako ni ndani ya wiki tu utaona mabadiliko.

pamoja na hayo mimi sio mtaalamu nimeongea tu kufuatia hatua nilizoona watu wakifuata na kufanikiwa
 
Perfume itakufanya unukie kwa muda tu lakin muda ukiisha kikwapa kiko pale pale. Jaribu kwanza kuondoa hio harufu pia ukiwa unaoga jaribu kusugua vizuri maeneo ya kwapani kwako itakusaidia.
Hayo manukato yawe ni sehemu tu ya kukufanya ujisikie vizuri na kukupa harufu nzuri.
 
Perfume utakufanya unukie kwa muda tu lakin muda ukiisha kikwapa kiko pale pale. Jaribu kwanza kuondoa hio harafu pia ukiwa unaoga jaribu kusugua vizuri maeneo ya kwapani kwako itakusaidia.
Hayo manukato yawe ni sehemu tu ya kukufanya ujisikie vizuri.
asante saana mkuu
 
Usiwe Mtu wa kufuga Nywele za KWAPA.

Jitahidi kufuta Nywele za KWAPA mara kwa mara kila zinavyoota.

Kila unapoenda kuoga sugua MAKWAPA yako na povu jingi la Sabuni.

Na ukishamaliza kuoga hakikisha unajikausha vizuri MAKWAPA yako, kisha tafuta kipande cha NDIMU au LIMAO ujipakaze kwenye MAKWAPA yako.

Kama bajeti yako inakuruhusu ukimaliza kuoga, jikaushe vizuri MAKWAPA yako kisha charazia DEODORANT.

Na sio MAKWAPA tu, na sehemu za siri pia jitahidi uwe unajikausha vizuri unapotoka kuoga.

Bila ya kusahau kuondoa Nywele za sehemu za siri pia.

Usiwe unaweka/unaacha Msitu
 
Back
Top Bottom