Wakuu nahitaji kununua gari naombeni ushauri wenu

Bajeti ndogo hyo huwezi pata gari used Japan ongeza mil.2 uagize nje ya nchi ka spacio, run x, au x_trial
 
Spacio ni gari nzuri Sana hata umbo lake siyo baya Kama la wish.ILA KAMA UKO VIZURI KIUCHUMI CHUKUA NISAN X TRAIL mafuta iko juu kidogo na service yake na vifaa vyake pia viko juu Ila haviharibiki haraka
Fuel consumption ya x trail ipoje mkuu
 
Kati hizo nimewahi tumia Wish na spacial Sitakaa nizisahau . Utumiaji wake mafuta kawaida but hazipendi Adha yan ukiituma zaidi ya km 20/30 inachemka vibaya service inakuhusu. Na pia ukiingia road za vumbi kwenye mawemawe utafurahi mwenyewe na ole wako pawe na matope. Zilichonikera zaidi hazitaki mizigomizigo yan ni special kwa round sasa kwa sisi wanakijiji tushazoea ukienda sehem ukikuta mbuzi ina bei nzuri unabeba, ukikuta mkaa unafunua siti unapakiza, ukikuta mihogo twende.
 
[emoji3][emoji3]du sasa kama 20km gari inachemka, sasa Mimi safari zangu za dar to njombe ntatoboa kweli...
 
Siyo hayo magari yalikua mabovu kweli? Yaani 20km gari inashika moto na ukahisi ni model nzima iko hivyo siyo kwamba gari zilikua na shida?
 
Bajeti ndogo hyo huwezi pata gari used Japan ongeza mil.2 uagize nje ya nchi ka spacio, run x, au x_trial
Nimepita pita kwenye wesbsite za kijapan za kuuza magari used. nimeona hizi x trail nyingi zinauzwa kuanzia 1500$ mpaka 1800$....kwamfano nikitaka niagize hii gari itanigarimu shingapi mpaka kuitoa pale bandarini
 
Samahani mkuu pale mwanzoni nadhani uliandika kitu kama hiki 'Mimi ni mtanzania mwenye maisha ya kawaida'.
 
[emoji23][emoji23]ni kweli kabisa mkuu hujakosea
πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ hio weka mbali na watoto,parts zake ni expensive kiaina kulinganisha na toyota ingawa ni genuine afu pia haliuziku fasta tofauti na toyota lkn ni gari poa sana ukifuata masharti yake.

X-trail ya 2003 itakua:
CIF yake ni Tsh. 5m+Kodi Tsh. 6.2m+other charges 1.2mil(hii nimeikadiria maana sio constant)=Tsh.12.4m

Yaani fanya mil 13. Unaiingiza road na umeshalipia kila kitu mkuu.
 
Nimepita pita kwenye wesbsite za kijapan za kuuza magari used. nimeona hizi x trail nyingi zinauzwa kuanzia 1500$ mpaka 1800$....kwamfano nikitaka niagize hii gari itanigarimu shingapi mpaka kuitoa pale bandarini
Ukitaka kuagiza gari angalia kwanza budget yako na kodi ya tra ipoje kwa gari husika maana kuanzia January hii kodi za magari zimepanda maradufu

IST saivi kodi yake imefika 6mil kutoka 4mil

Usipokuwa makini unaweza ukaagiza gari ukashindwa kuitoa bandarini
 
Nimepita pita kwenye wesbsite za kijapan za kuuza magari used. nimeona hizi x trail nyingi zinauzwa kuanzia 1500$ mpaka 1800$....kwamfano nikitaka niagize hii gari itanigarimu shingapi mpaka kuitoa pale bandarini
1500-1800usd Xtrail au?
 
Akiliacha bandarini ndo furaha ya jamaa zetu waleee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…