Wana JF siku za karibuni sukari imepanda bei sana katika ukanda huu wa Afrika Mashariki. Takwimu zinaonyesha sukari TANZANIA inauzwa kati ya Tsh 2,200/=($1.35)/ na Tsh 2,500/=($1.54) per 1-kg, KENYA Ksh 200 ($2.2) per 1-kg , UGANDA Ush 6,000/=(2.2)per 1-kg,na BURUNDI Fr 2,000/=(1.64)per 1-kg. Inashangaza kuona nchi zote za Afrika Mashari bei ya sukari ni ya juu sana. Wakuu naombeni kujuzwa ni kilichosababisha bei kupanda sana katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.
Kuna soko jipya South Sudan, hawa jamaa baada ya kupata Uhuru wakaacha kutegeme exports za North Sudan. Wajasiri amali wa eneo hili, hasa kutoka Uganda na Kenya walivamia soko hili jipya na kukausha baadhi ya bidhaa kwenye masoko yetu. Iwapo viwanda vyetu wangekuwa wamejipanga vizuri, basi hapa ndio ilikuwa nafasi ya kuwekeza zaidi lakini badala yake watawala wetu watakibilia majibu ya muda mfupi kama kudhibiti export ya sukari.