Wakuu naombeni mnifundishe formula ya kupika ugali

Wakuu naombeni mnifundishe formula ya kupika ugali

bright pledge 255

Senior Member
Joined
Aug 15, 2022
Posts
140
Reaction score
172
Wakuu naombeni mnifundishe formula ya kupika ugali ,maana kila nikipika unakuwa mbichi

vipimo vikoje ratio ya unga na maji

mda wa kusubiri kwenye kila stage

NITASHUKURU
 
Wakuu naombeni mnifundishe formula ya kupika ugali ,maana kila nikipika unakuwa mbichi

vipimo vikoje ratio ya unga na maji

mda wa kusubiri kwenye kila stage

NITASHUKURU
Badika sufuria yako ya maji ukitaka na ni vizuri.kwa wewe kukorogea uji usiwe mzito acha uchemke tu halafu weka unga endelea kusonga acha kidogo jikoni halafu ipua weka kwenye sahani tayari kwa kula

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Kama unakorogea hakikisha uji unachemka vizuri
Usitie unga mwingi kwa pamoja, tia kidogokidogo huku unaupa nafasi ya kuchemka
Ukishaona ugali unaelekea kuiva usiongeze tena unga hata kama unaona ni mlaini sana

Muhimu kuliko yote hakikisha moto upo wa kutosha. Kama unapikia mkaa, usitangulie kupika kitu kingine halafu ndio upike ugali, kama utafanya hivyo ni lazima uongeze mkaa kwanza, ukipikia moto uliopungua nguvu ugali hauivi hata ufanyeje
 
nimeshagundua makosa yangu huwa naweka unga mwingi kwa mkupuo pia nikiona ugali ni mlaini sana naongeza unga hata kama ni mwishoni
 
Ukiivisha kwa kufata maelekezo, utuwekee hapa tuonje tafadhali.
 
Moto uwe mkali, wacha uji uchemke, ongeza unga taratibu unaposonga ili uchanganyike vizuri ,ukimaliza uache jikoni kama dakika tano hivi mpaka usikie harufu ya unga kama una ungua flani hivi, songa kidogo kuuchanganya ,ukiona haunati kwenye mwiko. Epua kwenye sinia tayari kwa kula..

Ugali ulioiva huwa haunati kwenye mikono wakati unafinyanga tonge.
 
Back
Top Bottom