Naomba kufahamishwa kidogo kuhusu hii gari,kwa upande wangu naona ni gari nzuri kwa muonekano ni ndoto zangu kuja kumiliki hii gari, maana naona haizungumzwi sana katika hili jukwaa.
Naomba kufahamishwa machache kuhusu hii gari:
- Changamoto zake
- Ulaji wake mafuta
- Upatikanaji wa vipuri
- Na mengineyo
Hakuna haja ya kujiuliza mara2 hiyo gari iko poa kuanzia body yake, mashine na gear box, pia Corolla Fielder inatumia engine ya 1NZ ni engine zinazohimili Sana pia hiyo gari inafanana na pro box succeed.
Fasta Sana Fanya maamuzi wala haina haja ya kutafuta gari tofauti na hiyo
Unapokutana na brand yoyote ya toyota corolla iwe spacio, run x, fielder, axio etc hutakiwi kuuliza mara mbilimbili, we angalia shape tu kama inakupendeza machoni ichukue, hazinaga stress hizo gari.