Wakuu nipeni ushauri kuhusu puppy (mbwa mdogo)

Wakuu nipeni ushauri kuhusu puppy (mbwa mdogo)

Its Pancho

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
15,966
Reaction score
26,404
Wakuu,

Kambwa hako nimepewa na ndugu yangu mmoja anao wengi sana, halafu bado Kana afya nzuri sana.

Naomba mnipe ushauri jinsi ya kumtunza vizuri kuanzia chakula gani ale jamaa aliniambia huwa bado kadogo kanakunywa maziwa tu.
Hivyo siku ya pili hii nakaptia maziwa.

Nataka akue vizuri na kubaki na afya yake hivyo hivyo. Na bao langu(mtoto wangu) anapenda sana ndo maana nikamleta. Banda tayari lipo kubwa.

Je, matunzo, ale chakula gani? ,dawa?

Nifanyeje ili asiwe mzembe?
 
Yaani wewe unatoka darasani, unakuja kuuliza maswali mtaani?

Kwa nini usimuulize huyo ndugu yako akakupa maelezo yote muhimu jinsi alivyo fanikiwa kuwalea vizuri na hata kuwazalisha wakawa wengi?

Mwisho: kama hilo likishindikana au ukikosa majibu muafaka hapa, tafuta Bwana mifugo mtaani kwako atakuekeza kila kitu
 
Yaani wewe unatoka darasani, unakuja kuuliza maswali mtaani?..
Kama huna la kujibu ni vyema ukakaa kimya.

Hapa kuna wataalam zaidi ya huyo jamaa, na zaidi kuna wataalam wa mifugo rundo hapa.

Ikifikia stage humu unayotaka kwamba kila mtu mwenye shida asiulize hapa akaulize mtaani. Utakuwa umepungukiwa madini kidogo kichwani..

Samahani
 
Umeuliza swali zuri...Je anaumri gani?ni aina gani ya mbwa?kama amezidi wiki 4 muulizie kama amempa chanjo ya DHLP?Dawa ya minyoo pia.Naomba tuanzie hapa na kwaushauri nichek 0686 666666 mimi pia nafuga mbwa
 
Mkuu hata sijui ni aina gani kwa kweli
Lakini nitaweka picha zao na pia nitakutafuta kwa namba hii uliyoweka

Nashukuru
 
Back
Top Bottom