Wakuu!! Njooni hapa tuongee na Fareed kubanda (Fid Q)

Nakubaliana na wewe ,wengi hawajui business, hasa kutumia hizo social media, but Fid Q narudia tena jamaa ana project zake nzuri tu

Tatizo ni yy kujiamini kupita kiasi,kujifanya mjuaji wa kila kitu. Nimewahi kufanya naye kazi ktk hizo project ,najua tatizo lake
 
Ushauri bora kabisa sina cha kuongeza maana tukiongeza hapa atashindwa kujua aanze na lipi.. kama kuna mtu anamfahamu amfikishie ujumbe huo..... haoni hata wenzie kna FA na AY walivopiga hatua ? Aachr ungosha ngosha sana kama hawezi kujisimamia atafute manager tu mzuri ambaye yuko updated na dunia ya muziki wa sasa wapige biashara ye abakie kutunga mashairi tu then manager akomae kutekeleza hizo vision hapo juu..

Binafsi nilishaanza kumpotezea huyu jamaa baada ya kuona ni mtu wa kupelekwa sana na media af hajui ni jinsi gani ana uzito kwa mashabiki....

Anafurahia kupakwa kwenye coaster tu na mazombie wengine na kirusha selfie....

Komaa bana mwanamalundi dn let us down....
niko hapa naskikiza ngoma yako JUHUDI za wasiojiweza ft Bi Kidude
 
Tatizo ni yy kujiamini kupita kiasi,kujifanya mjuaji wa kila kitu. Nimewahi kufanya naye kazi ktk hizo project ,najua tatizo lake
Hilo ndio tatizo Kuu, nimewahi kuwasiliana na hawa wanamuziki kadhaa wa Tamaduni kuhusu namna bora ya wao kuuza bidhaa zao za sanaa na matumizi sahii ya social media, nikagundua ni watu wanapuuza ushauri, na ujuaji mwingi. Kwa maoni yangu sidhani kama msanii mwenye kipaji anahitaji kulia shida ndani ya nchii hii.
 
"leta kiburi uchinjwe watu wale kichuri..."//

"Fidq akiwitness ninavyopata sifuri..//"

[emoji115]

Maneno Ya Nikki mbishi baada ya kuambiwa na fidq kuwa hana nidham
 
Sio Fid q tu hata wasanii wengi tu kama Ruby , Q chillah , Ray c, Marlaw ..bado wana uwezo lakini hawajui kwa sasa nguvu ya clouds na wasafi ni marketing and branding. Hii ndo maana league ya diamond na Ruge ni ya moto kwa kuwa wote wanacheza ground moja ila diamond naye asingekuwa na team iliyoshiba nyuma yake plus mitandao , mbona angekuwa kashapotezwa kitambo..
Angalia wasanii yaani kila mmoja anajaribu kuwa kama diamond au vanessa mdee na kusahau zile ni brand zao na unapoziiga unawanufaisha wao na si yeye..

Wasanii waache ujuaji mwingi maana wanatakiwa kutafuta watu wa marketing, branding na PR..wao watengeneze muziki mzuri alafu waache wengine wacheze na soko kama diamond anavyofanyiwa na akina salaam, babu tale na fela yaani hata nguvu ya clouds imeegemea huko huko..
MOBETTO kashtuka na kamuajiri dada wa kikenya kwa shughuli hiyo na ndo maana anapiga pesa huku wenye vipaji wamezubaa tu ..hakuna UCHAWI HAPA

Nikimuangalia Ruby kwa sauti aliyonayo, muziki anaouimba na lifestyle yake ni maji na mafuta , hapo ndo najua hata kama ana manager mwenye pesa lakini bado hazijui SIRI za mchezo ...WASANII WAHESHIMU NAFASI ZA WATU , WAIMBE HALAFU SOKO WAWAACHIE WENYE UWEZO NALO
 
Bro Mimi ni msanii samahan unaweza nisaidia nikapata konection japo mbili Tatu ninazo ngoma nazaz mwez ujao nitashoot video sasa shida inakuja kwenye konection tu
 
"yulee usimuache ruby achuje...//

Salam Kwa nape mnauye..' kama mnapenda asali Kwa nini nyuki mtutenge...??//

Nikki mbishi aliona mbali sana nakuwasilisha sanaa yake vyema akiwa na maana kuwa wasanii wana nyonywa sana

[emoji115]Ukisoma mstari wa hapo juu hapo kwenye 'yulee" Ana maanisha "Ruge"

Ilibidi aseme "rugee usimuache ruby achuje ....//

Nikki mbishi anajielewa sana.
 
Kuna mtu anaitwa Nikola Tesla. Kwangu mimi huyu ndie mwanasayansi bora zaidi kuwahi kutokea.

Alikua na kipaji cha ajabu, yani jamaa aliweza kuvuna umeme out of thin air. Na yeye ndie msingi mkuu wa wireless communications tulizo nazo sasa.

Pamoja na kipaji chote hicho, jamaa alikufa akiwa masikini huku wajanja kama Thomas Edison wakipiga hela kutumia gunduzi na tafiti zake!

Sababu ni moja tu, alifeli kujitengeneza as a business brand, akamuuzia Thomas Edison patents za ugunduzi wake!

BACK TO THE TOPIC!

Mtu yeyote anaefuatilia hip hop hawez kuutilia shaka uwezo au kipaji cha Fid Q. He's simply on his own level.

Tatizo ni moja tu, haelewi nguvu ya brand katika biashara. Hapa naweka scenario kadhaa kuthibitisha hoja yangu.

1. Amekua mtu wa teams hapa karibuni.

Unaikumbuka remix ya Fresh akiwa na Diamond na Ray vanny? Unakumbuka vile Diamond aliutumia wimbo huu kumdis Ali kiba?
That was a very stupid move kwa upande wa Fid Q.

Kwa heshima yake hakutakiwa kuruhusu wimbo wake utumike kumdis msanii mwingine ambae yeye hahusiki na ugomvi wao.

Unadhani leo Ali Kiba anaweza kufanya collabo na Fid Q kirahisi baada ya kuisikiliza fresh remix? Mimi sijui, ila pale kaka mkubwa alichafua brand yake.

Kama vile bado haitoshi, sasa hivi kaamua kua team Clouds huku akitupiana maneno na Wasafi. Kulikua na ulazima gani? Kwani asingeweza kupiga show fiesta bila kutupiana maneno na Wasafi?

Je, unadhani anaweza
tena kufanya project na Wasafi? Mimi sijui, ninachojua ni kwamba kaka mkubwa kaharibu kwa Ali Kiba (collabo ya fresh) na sasa kaharibu kwa Diamond kwa sababu ya kupenda u-team usiokua na manufaa!

2. Amekua cheap sana ukimlinganisha na status yake!

More than ten years in the game, bado kaka anapiga show za laki kadhaa au milioni moja. Ni aibu kumuona Fid Q akiwa kwenye coaster anaenda kupiga show Muleba, unafikiri akina Young killer na Dogo janja wanajifunza nini kutoka kwake?

Kwa status yake angeitambua nguvu ya branding, sasa hivi angekua anaandaa shows zake then yeye ndie awaalike vijana akina Young killer waje kussuport.

Badala yake, ameamua kubanana nao kwenye coaster ya Tigo fiesta. PATHETIC!

MWISHO;
Tuko kwenye zama za ubepari. Kua na kipaji pekee haitoshi. Bila kua na mipango mizuri ya kibiashara utabaki kulalamika na kutoa ngoma kali ambazo hazikulipi.

Hebu waangalie Navy Kenzo, wakikutana na Ali kiba wanacheka nae then wanaingia studio wanatoa ngoma. Kesho wakikutana na Diamond wanacheka nae, wanaingia studio wanatoa ngoma. Habari ya teams wamewaachia wenyewe!

Kama Diamond asingeitambua nguvu ya branding pengine asingeweza kupiga mkwara miaka ile kwamba bila milioni kumi sifanyi show, wakati wenzie walikua wanapiga show za laki tatu.

Pengine na yeye angekua kwenye Coaster ya fiesta hivi sasa. Ngoja niishie hapa, maana maneno yanakuja tu kichwani hayaishi.

[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Simply perfect analysis. We jamaa kichwa chako huwa kimetulia sana. Nimekuelewa kwa urahisi sana.

[emoji818][emoji109]
 
Uwo ni mtazamo wako binafsi ...wabongo manakasolo kubwa yakujifanya mnataka kumjua mtu sana ...Fid q ni msanii anayejitambua . na yeye awez akwakwambia anamiliki nini ...hapa mjini ..kwa hilo namshukulu fid q kutofautisha maisha yake binafsi na maisha yamziki.

Uwezi kumongelea msanii kama Fid q aliyedumu kweny mziki miaka 18 akiwa kweny chart ...mtoa uwo ushauri kampe chid Benz na wala sio fid q.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…