Wakuu Tuifatilie Toyota belta

CHIBA One

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2018
Posts
558
Reaction score
2,093
Hii ni gari ambayo nimekuwa mara nyingi naifatilia tu mtandaoni.... Gari hii inatengenezwa japan na ilianza kutengenezwa kati ya mwaka 2005 hadi 2012 production yake ikasitishwa. Model ya mwaka 2006 ni kama continuity ya platz.. Na ukiangalia engine yake ni cc 990 related to vitz na gari zingine ambazo ni very economy in terms of fuel

Mwaka 2008 ikaja model ambayo ina cc 1290 ambayo kimuonekano ni sawa na premio ya 2008 Au jamii ya magari hayo Kama avensia, verossa na zingine!

Gari hii sijaiona kabisa bongo japo kwa macho inavutia kwa kweli na Ina kila sifa za gari ya kutembelea in terms of muonekano mzuri, comfortability kwenye seats na matumizi madogo sana ya mafuta.

Imenivutia Na nnataman wajuzi au waliowahi kuitumia watupe uzoefu.



Sent using Jamii Forums mobile app
 



Nadhani itakua nzuri kwa wazee wa engine ndogo ndogo.

Nimecheki Beforward naona CIF nyingi ni below $2500 na ushuru wa TRA ni Mil 5.7 so ukiwa na Mil 12 unaagiza hii gari.
 
Nairobi zinafanywa UBA kama ilivyo IST hapa bongo pia uzuri wake hizi belta ni nafasi yake kubwa ndani kuanzia family na biashara inafaa Sana .
Dar zipo nyingi tena muda mrefu zipo mtaani
 
Daah hio belta ukija platz zote zina sura mbaya tu mazee.
 
TOYOTA. BELTA

Kama unafikiria sana kununua gari kama ni kijana nakushauri nunua toyota belta kutokana na uwezo wake hasa kwenye mafuta iko vizuri mno , upande wa umbo la gari ni saloon lkn pia ni gari ambayo ni stahimilivu japo ni adimu sana

Washindani wa gari hii kwenye soko ni. Honda Fit Aria, Nissan Tiida, na Toyota Axio
Upande wa ndani inakuja na
[emoji108]Umbo la gari ni Saloon
[emoji108]Extras: Rear Spoiler
[emoji108]Safety Features: ABS, Curtain
[emoji108]Airbags, EBD, SRS Airbags, TRC, VSC
[emoji108]Exterior Features: Alloy
[emoji108]Rims(optional), Fog Lights(optional)
[emoji108]Interior Features: 12V 120W Power Output, CD/Radio player

MAELEZO
Toyota Belta Ilianza kuzalishwa mwaka 2005 na uzalishaji wake ulikoma mwaka 2012. generation hii inajulikana kwa jina la SCP9/NCP9 na iko based kwenye platform kama ilivyo second generation Toyota Vitz. Kuhusubtairi za gari hij ni kubwa kuliko za vitz upande wa ndani ina mvuto wa hali ya juu sana

Upande wa injini

Toyota Belta inakuja na machaguo matatu ya injini 3 ambayo ni
[emoji91] 1.0 Litre 1KR-FE engine,
[emoji91]1.3 Litre 2SZ-FE engine
[emoji91] 1.3 Litre 2NZ-FE engine(for 4WD models).

Upande wa transmition
i) Super CVT-i transmission for the 2WD models
ii) Super ECT transmission

Gari hii inakuja na grade mbili lakini zikiwa poa sana hebu tuone
[emoji108]Toyota Belta Grades

[emoji91][emoji91] Toyota Belta X – Toleo la grade hii ni la kwaida linakuja na 1.0L engine au 1.3L engines, 2WD/4WD, halogen headlights, basic speedometer gauge, keystart, 14-Inch steel rims na manual AC.

[emoji91][emoji91]Toyota Belta G – Toleo hili ni luxury grade linakuja na 1.3L engines, 2WD/4WD, xenon headlights, upgraded speedometer gauge, chrome trim, keyless/smart start, 15-Inch alloy rims, turn signal on side mirrors, luggage cover, padded seats na automatic AC.

Uchague lipi ? Kama unakipato cha mawazo au kama haujawahi kumiliki gari yoyote toka umetoka tumboni mwa mam yako nakushauri nunua Grade ambayo ni TOYOTA BELTA X....ni rahic sana kulimudu kuliko luxury ....japo la luxury linafaa sana kama ukiwa mtu wa safari sana utaenjoy

Toyota Belta Interior
Kwa upande wa ndani imepangiliwa vizuri sehemu ya kuweka miguu kwa upande wa mbele inananfasi kubwa ila kwa vitu vya nyuma kwa mtu ....anaweza kupata shida kwa muda mrefu kusafiri kama mtu ni mrefu anashauriwà akae kiti cha mbele ambacho kina nafasi kubwa , upande wa dashboard imewekwa vizuri ipo katika hii inasaidia wote walio ndani ya gari kuona mwendo na uunapoishiwa mafuta wote wanaona ...inakuwa rahic kuwaomba hela ya mchango wa mafuta [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Toyota Belta Exterior
Kwa upande wa nje , Belta inaelekea kufanan na Axio. Higher grades inakuja na alloy rims na fog lights.

Upande wa acceleretion

[emoji108][emoji108]Toyota Belta 1.0L accelerates inatoka 0-100 km/h kwa 15.4 sec.

[emoji108][emoji108] Toyota Belta 1.3L accelerates inatoka 0-100 km/h kwa 13.5 sec.

Hebu tuone upande wa mafuta iko vipi yaani hapa toyota [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nawapa pongezi mmejua kunikosha walahi hebu tuone

[emoji108] Toyota Belta 1.0L inatumia km 22.5 Kwa lita 1

[emoji108] Toyota Belta 1.3L 2WD inatumia km : 20.0 Kwa lita 1

[emoji108] Toyota Belta 1.3L 4WD inatumia km : 16.0 Kwa lita

Upande wa tank ni lita 42 ... Tu
Gari hii nimeipendea sana mafauta iko vizuri hasa kama unafanya biashara ya uber halafu gari iwe yako !! Lazima utoke shavu

GROUND CLEARENCE
Upande wa uvungu wa gari inakuja na 5.9 inch sawa na sawa na 150 mm kwa kuwa umbo lake ni dogo unaweza kuisogeza mpk 6.3 inch ukizidisha unaharibu center of gravity ya gari

Toyota Belta Stability and Handling
Upande wa injini ya 1.0 inahitaji uvumilivu kwa kuwa inamwendo mdogo na pia kwenye upandaji wa milima gari hii ipo slown sana
Injin ya 1.3 inaonyesha kidogo kiwa na mwendo lakini sio mkali kiujumla ni gari yenye mwendo wa wastani

Matunzo ya gari
Utasoma katika manuala ya gari ile ya kijapani tuliza akili wakati wa kuisoma maana wajapani wanajua kuwaweza watu sio kwa kijapn kile

Kwa nini ununue gari hii
[emoji108].inamatumizi mazuri sana ya mafuta
[emoji108]Inafaa kwa watu wa kipato kidogo
[emoji108]Service zake ni gharama ndogo sana
[emoji108]Gharama yake ya kuinunua ni ndogo

Changàmoto katika gari hii ni
.upande wa gear box inazingua sana kutokana na mazoea ya uwekaji wa oil ambayo haijashauli na watengenezaji wa gari , kuwa makini sana kwenye Transmition oil gear box yake ipo sensitive

[emoji108]Engine failure hasa kwa injini ya 1.0
Ukitaka kudumu na gari hili weka ujuaji wako pembeni soma manuala ya gari hata kama ni kijapani ww soma [emoji23][emoji23]

[emoji108]Unstable at high speed

Conclusion
The Toyota Belta is essentially a saloon version of the Toyota Vitz and therefore appeals to the same demographic. It’s ideal for people that value reliability, fuel efficiency and easy maintenance
 
betla tukiweka mafuta ya ten tunazurula ad unahc utapotea kagar kazur sana aka kwa vjana waunga noti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…