Wakuu tujadiliane,ni shughuli zipi ambazo utatumia mtaji mdogo kwa kuongezea thamani vitu/huduma na kuviuza kwa bei ya faida?


Nunua mahindi jioindi Cha msimu wake kwa Bei cheap,pack kwenye mifukoni ya kg1,2
 
Ila kiukweli bidhaa nyingi hapa tanzania hasa za kilimo zinahitaji sana kuongezewa thamani ili ziende mbele,Tanzania tuna packaging mbovu mno kwenye bidhaa zetu na hatuna elimu ya kutosha kwenye kufanya grading,sorting,screening na packaging ukiachilia mbali vikwazo kwenye export.

Tunahitaji angalau kwenye shule zetu kama veta na hata vyuo vikuu kuwe kuna kozi za ngazi mbali mbali zinazohusiana packaging.

Unakuta mtu kasindika korosho halafu ndani zingine zimeungua,zingine zimevunjika,zingine nusu nusu halafu anataka kupeleka nje ya nchi na hata nutritional content hajaandika wala expiry date haipo.

Value addition kwenye mazao ya kilimo bado kuna fursa nyingi na kunalipa tukiamua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Sido hua wanajitahid kuandaa semina lakini bado sana!...yaani bado mno!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…