Wakuu uskani (Steering) wa gari langu umejifunga msaada wa haraka

Kasinja jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2017
Posts
1,034
Reaction score
1,812
Jana baada ya mizunguko yangu, nikazima gari vizuri tu, sasa Leo naweka ufunguo kuwasha hata hauzunguki,

Nikajaribu kuzungusha steling nasikia kama imebana haitoki, nikajua hapa steling imeloki,

Msaada naifunguaje,

Gari ni Voxy
 
Ina maana huo ufunguo uliotia sio wake? Na italokije wakati kuna ufunguo ushauingiza..
 
Don' laugh, school him/her.
Mbaya zaidi situation kama hiyo inakukuta umeshawapita watu hujawasalimia,umechomekea mwenyewe unatembea kwa mapozi utafikiri unaenda kuendesha Ferari,halafu unakwama kwenye kuunlock steering,hapo nina uhakika lazima jamaa alivyoingia kwenye gari hakutoka,akaanza kutafuta msaada JF huku kajifungia ndani akitaabika kwa joto ili asionekane kuna kitu kinamshinda,na mpaka anapata ufumbuzi kama ni Dar lazima shati akamue jasho...
 
Tumejua mkuu umrpata voxy zama za Magu, ingekuwa vipindi vingine ungechomoa kama la mshana jr
 
Mbaya zaidi situation kama hiyo inakukuta umeshawapita watu hujawasalimia,umechomekea mwenyewe unatembea kwa mapozi utafikiri unaenda kuendesha Ferari,halafu unakwama kwenye kuunlock steering,hapo nina uhakika lazima jamaa alivyoingia kwenye gari hakutoka,akaanza kutafuta msaada JF huku kajifungia ndani akitaabika kwa joto ili asionekane kuna kitu kinamshinda,na mpaka anapata ufumbuzi kama ni Dar lazima shati akamue jasho...
Hahaha! Pozi lote linaisha.
 
Hahahaaaaa!! Umenikumbusha tukio ndugu!!!

Kunau dada duu mmoja aliingia kwenye gari yake vits new model! Akashangaa sterling ipo kama imeng'ooka alihamaki huyo ila hakutaka ajulikane.

Bahati nzuri mie huwa ni mtu wa masihara na matani popote pale na huwa natania yeyote!!

Nimepita kwenye gari yake nikakuta yumo ndani ya gari ila mguu mmoja upo nje kuweka mlango wazi! Nikamzingua kwa style aliyokaa huku napita zangu kufuata langu nikasikia 'eheeee!! Kaka kakaaa hebu njoo gari yangu kuna mtu kailegeza sterling sijui ana maana gani?'

Ili kumrudisha awe normal nikamtania tena halafu nikamwambia nipishe leo nikupeleke kwenu we kaa kwa abiria!! Nikamuonuesha na kumuelekeza jinsi sterling lock inavyofanya kazi!!

Alifurahi kinoma, akasema leo nisingeenda nyumbani bora hata ulipita ukaniongelesha nikapata nguvu ya kukuuliza!! Nilishachanganyikiwa!!

Nikikumbuka jinsi macho yalivyokuwa yamemtoka yule dada akiamini kuna mtu kangoa sterling yake napata picha ya huyu jamaa mpaka kuja JF 😂😂😂😂 kuongea na watu ni muhimu sana jamani!! Mie huwa sijivungi, yeyote na popote mie twende kazi na nipo hivyo tangu na tangu ni rahisi kupata msaada popote!!
 
Back
Top Bottom