Wakuu wa wilaya za mkoa wa Tabora wameiomba serikali kuwajengea nyumba za kuishi pamoja na ofisi zao, wakieleza kuwa kwa sasa wanatumia majengo chakavu na ya zamani. Baadhi ya majengo hayo hujaa maji pindi mvua zinaponyesha, hali inayodhoofisha mazingira yao ya kazi na kuonyesha kutokuwepo kwa hadhi inayoendana na nyadhifa zao.
Wakuu hao wa wilaya, wakiwemo Mohamed Mtulyakwaku wa Wilaya ya Uyui, Mhandisi Deusdedith Katwale wa Wilaya ya Tabora, na Bi. Sauda Mtondoo wa Wilaya ya Igunga, walitoa hoja hiyo wakati wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichojadili na kupitisha mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026.
Si wajenge nyumba zao au waendelee mtaani wakapange
Ikishindikana warekebishe zisivuje kwa gharama na faida zao.Washukuru hata wanakaa nyumba za bure zilizojengwa kwa kodi zetu wavuja jasho