vamda
JF-Expert Member
- Aug 1, 2012
- 895
- 571
Ndugu wana JF. Nimegundua wakuu wengi wa shule hupenda kuabudiwa kwa kujifanya miungu watu mashuleni. Nimeyaona haya kwenye shule kadhaa za sekondari. Endapo kuna walimu wanaopenda ukweli na uwazi huchukiwa na uongozi wa shule. Mfano walimu wakitaka kujua mchanganuo wa mapato na matumizi ya fedha za shule,au wakitaka kufahamu kuhusu fedha za miradi ya shule huchukiwa sana. Walimu hao watafanyiwa vitimbi mbalimbali vikiwemo kunyimwa fursa ya kusimamia/ kusahihisha mitihani ya kitaifa ,kuhudhuria semina n.k. Wakuu wengi wa shule huwazushia maneno ya uongo (majungu) walimu hao kwa maafisa elimu ambao nao kwa kukengeuka wengi wao hupenda kusikiliza na kuyaamini maneno ya wakuu wa shule (MAJUNGU). Wana JF naomba mfunguke kuhusu madhila haya wanayotendewa walimu wanaopenda maendeleo mashuleni. Je, hii ni HALALI?