Unauliza "mbona serikali wazito namna hii" kana kwamba swala hilo ni cut-and-dry na wote government, parliament and Tanzanians at large tunakubaliana tunataka uraia pacha. Sivyo.
Kuna mgawanyiko mpana kwenye jamii juu ya swala la kugawa uraia wa Tanzania kwa watu wengine, serikalini pia kuna wide division, kumbuka Wizara ya Mambo ya Ndani na Foreign Affairs walivyotoa misimamo inayosigana mwaka jana.
For any number of reasons. It is not very clear what benefits will be reaped by mkulima na mfanyakazi wa Tanzania kwa kuleta uraia pacha. Au, critics wamesema, watakaonufaika ni wageni, kama Wahindi na Waarabu na Wakenya, ambao watatumia mwanya huo ku exploit economic privileges za Mtanzania.
Hoja ya wanaoomba uraia pacha ile iwawezesha kuwekeza "nyumbani" nayo inagonga gonga ukuta, wameulizwa ni kitu gani ambacho huwezi kuwekeza bila uraia? Mchina anawekeza kwenye mikokoteni ya kukusanya chuma chakavu Kariakoo, Mmarekani amewekeza kwenye kuzalisha umeme Ubungo, Mhindi amewekeza kwenye maduka na ufisadi mjini, wewe Mswahili uliyezaliwa Kariakoo ukachukua uraia wa India hapana shaka utaweza kushindana na Wachina na Wahindi kuwekeza "nyumbani" na uraia wako wa India.
Wanaohoji uraia pacha pia wame question uzalendo wa Watanzania ambao waliutema uraia wa Tanzania walipohamia ughaibuni na sasa wanautaka tena, Rais Kikwete alisema "wanataka kula huku na kule."
Mwisho wa siku, hata kama kuna faida lukuki, swala la uraia pacha sio priority agenda ya nchi kwa sasa and is not in the conversation. Katika immigration policy na citizenship framework kwa ujumla kuna imperatives nyingine zinazotuumiza vichwa kwa sasa, immigration dynamics za East African integration, national identity cards za Watanzania, na more pressingly, uraia wa Watanzania uchukue sura gani kama katiba mpya ita overhaul Muuungano. Hayo ndio tunayo grapple with on the nationality front, sio uraia pacha.