Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Habari zenu Wakuu wenzangu naomba kuuliza Swali hili je Sheria za Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, kuhusu Mtanzania kuwa na Uraia wa nchi mbili hapo kwetu imepitishwa na Serikali yetu? Na pia ningeomba kama kuna Mtu ana kitabu cha Sheria ya Jamhuri wa Muungano au Katiba ya Serikali ya Tanzania naomba anipatie Naomba hilo swali langu nijibiwe asanteni
mimi sipo Dar es-Salaam ndio maana nikataka kujuwa kuhusu hilo suala je wamelipitisha Wabunge? au ndio limewekwa kapuni? Au ndio Tungojee Serikali mpya ya mwaka 2015?Sheria ya uraia wa nchi mbili bado haijapitishwa.Hata hivyo kwakuiwa tunayo sheria kuhusu uraia(The Citizenship Act),kuna uwezekano isiwepo sheria mpya badala yake ikliyopo itafanyiwa marekebisho.Kuhusu katiba mimi ninayo copy moja,ila kama uko Dar es Salaam,waweza kwenda duka la Serikali lililoko mtaa wa Jamhuri na kujipatia copy yako kwa bei ndogo tu.
Habari zenu Wakuu wenzangu naomba kuuliza Swali hili je Sheria za Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, kuhusu Mtanzania kuwa na Uraia wa nchi mbili hapo kwetu imepitishwa na Serikali yetu? Na pia ningeomba kama kuna Mtu ana kitabu cha Sheria ya Jamhuri wa Muungano au Katiba ya Serikali ya Tanzania naomba anipatie Naomba hilo swali langu nijibiwe asanteni
Kama ndio hivyo basi bado sisi Wa Tanzania tupo nyuma sana Kimaendeleo tunazidiwa hata na majirani zetu itabidi Serikali ilifikirie kwa upya hili suala la kuumpa Mtanzania nafasi ya kuweza kumiliki Uraia wa nchi mbili kwa wakati mmoja.hakuna sheria inayoruhusu uraia wa nchi mbili, kuhusu katiba tembelea website ya bunge Parliament of Tanzania.(click hapo kwenye parliamnet)
Serikali inachongojea nini hili suala Bila ya kulipitisha? Au ndio mpaka tungoje tena wakati wa kampeni ya Uchaguzi mkuu mwaka 2015 ndio walizungumzie hili suala ndani ya Kampeni? mbona wamekuwa wazito namna hii hao viongozi wa Serikali?Sheria kuhusu suala la Mtanzania kuwa na uraia wa nchi mbili bado haijapitishwa....Unaweza ku download katiba ya Tanzania kupitia website ya bunge hakikisha unatafuta na Amendment bill ya constitution
Unauliza "mbona serikali wazito namna hii" kana kwamba swala hilo ni cut-and-dry na wote government, parliament and Tanzanians at large tunakubaliana tunataka uraia pacha. Sivyo.Serikali inachongojea nini hili suala Bila ya kulipitisha? ... mbona wamekuwa wazito namna hii hao viongozi wa Serikali?
hao uliowataja ( Wahindi na Waarabu na Wakenya, ambao watatumia mwanya huo ku exploit economic privileges za Mtanzania. ) Wapo wangapi hapo kwetu Tanzania? Wanaweza kufika Watu Millioni moja?walishindwa kuharibu Uchumi wa Tanzania baada ya kupata Uhuru mpaka sasa Wataweza kuharibu sasa eti kwa sababu ya kuwa na Uraia wa nchi mbili kwa wakati mmoja? MkuuUnauliza "mbona serikali wazito namna hii" kana kwamba swala hilo ni cut-and-dry na wote government, parliament and Tanzanians at large tunakubaliana tunataka uraia pacha. Sivyo.
Kuna mgawanyiko mpana kwenye jamii juu ya swala la kugawa uraia wa Tanzania kwa watu wengine, serikalini pia kuna wide division, kumbuka Wizara ya Mambo ya Ndani na Foreign Affairs walivyotoa misimamo inayosigana mwaka jana.
For any number of reasons. It is not very clear what benefits will be reaped by mkulima na mfanyakazi wa Tanzania kwa kuleta uraia pacha. Au, critics wamesema, watakaonufaika ni wageni, kama Wahindi na Waarabu na Wakenya, ambao watatumia mwanya huo ku exploit economic privileges za Mtanzania.
Hoja ya wanaoomba uraia pacha ile iwawezesha kuwekeza "nyumbani" nayo inagonga gonga ukuta, wameulizwa ni kitu gani ambacho huwezi kuwekeza bila uraia? Mchina anawekeza kwenye mikokoteni ya kukusanya chuma chakavu Kariakoo, Mmarekani amewekeza kwenye kuzalisha umeme Ubungo, Mhindi amewekeza kwenye maduka na ufisadi mjini, wewe Mswahili uliyezaliwa Kariakoo ukachukua uraia wa India hapana shaka utaweza kushindana na Wachina na Wahindi kuwekeza "nyumbani" na uraia wako wa India.
Wanaohoji uraia pacha pia wame question uzalendo wa Watanzania ambao waliutema uraia wa Tanzania walipohamia ughaibuni na sasa wanautaka tena, Rais Kikwete alisema "wanataka kula huku na kule."
Mwisho wa siku, hata kama kuna faida lukuki, swala la uraia pacha sio priority agenda ya nchi kwa sasa and is not in the conversation. Katika immigration policy na citizenship framework kwa ujumla kuna imperatives nyingine zinazotuumiza vichwa kwa sasa, immigration dynamics za East African integration, national identity cards za Watanzania, na more pressingly, uraia wa Watanzania uchukue sura gani kama katiba mpya ita overhaul Muuungano. Hayo ndio tunayo grapple with on the nationality front, sio uraia pacha.
Na nyinyi mlioko uhamishoni mnaoomba tuwakubalie uraia pacha, mko wangapi?hao uliowataja ...ambao watatumia mwanya huo ku exploit economic privileges za Mtanzania. ) Wapo wangapi hapo kwetu Tanzania?